Pata taarifa kuu
ALGERIA-CORONA-AFYA-RAMADHANI

Covid-19: Algeria yafunga biashara kwa sababu ya ukosefu wa nidhamu

Biashara nyingi, zilizofunguliwa tena wiki iliyopita, zimefungwa tena tangu mwishoni mwa wiki hii iliyopita katika maeneo kadhaa nchini Algeria, kwa sababu ya kutofuata kanuni za usafi na hatua ya kutokaribiana kwa umbali wa mita moja, kwa mujibu wa mamlaka.

Soko la wilaya ya Khraicia, kusini mwa Algiers, Aprili 25, 2020.
Soko la wilaya ya Khraicia, kusini mwa Algiers, Aprili 25, 2020. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangu kuanza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani zaidi ya wakuu 15 wa majimbo kati ya 48 wamejikuta hatua walizochukuwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona hazitekelezwi na wafanyabiasha pamoja na raia katika majimbo yao, na hivyo kuagiza kufungwa kwa biashara zote, hasa maduka ya nguo, maduka ya viatu, migahawa na maduka ya mikate, yanayotembelewa sana wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, pamoja na maduka ya manukato.

Picha za milolongo ya watu wakiwa mbele ya maduka zimewakasirisha viongozi na maafisa wa afya.

Zaidi ya vifo 460 vimerekodiwa nchini Algeria tangu kuripotiwa kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya Corona, Februari 25, kulingana na Kamati ya kisayansi inayofuatilia jinsi ugonjwa huo unavyoendelea nchini.

Jumla ya kesi 4,474 za maambukizi zimetangazwa rasmi.

Lakini tangu kuanza kwa mfungo wa mwezi mtakatifu wa Ramadhani Aprili 24, vifo 56 na kesi mpya 1,467 zimetangazwa.

Siku ya Ijumaa rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune alitishia kuongeza masharti ya raia kutotembea ikiwa hatua za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona zitapuuziwa.

Aliporuhusu maduka kufunguliwa tena wiki iliyopita, Waziri Mkuu Abdelaziz Djerad aliwataka raia wa Algeria "waendelee kuwa uangalifu kwa kuheshimu kanuni za usafi, hatua za kutokaibiana kwenye mbali wa mita moja na kujilinda".

Tangu Aprili 24, mamlaka nchini algeria imelegeza masharti ya watu kuttotembea katika wilaya tisa nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.