Pata taarifa kuu
ALGERIA-CORONA-AFYA

Kesi ya kwanza ya maambukizi ya virusi vya Covid-19 yatangazwa nchini Algeria

Mamlaka nchini Algeria imetangaza kwamba kesi ya kwanza ya maambukizi ya virusi vya ugonjwa hatari unafahamika sasa kama Covidi-19 imegunduliwa katika ardhi ya nchi hiyo.

Moja ya mitaa ya Algiers mwaka 2015.
Moja ya mitaa ya Algiers mwaka 2015. wikimedias commons
Matangazo ya kibiashara

Baada ya Misri wiki mbili zilizopita, Algeria inakuwa nchi ya pili katika bara la Afrika kukumbwa rasmi na janga hilo.

Waziri wa Afya wa Algeria amethibitisha kesi hiyo Jumanne wiki hii katika taarifa ya habari ya ya jioni kwenye televisheni ya serikali.

Virusi hivyo viligunduliwa kwa raia wa Italia aliyewasili nchini Algeria Februari 17, 2020, amesema waziri wa Afya wa Algeria.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, mfumo wa upimaji uliowekwa ndio umewezesha kugundua watu wawili ambao wanashukiwa kuambukizwa virusi vya Covid-19, lakini baada ya kufanya vipimo mtu mmoja ndiye alipatikana na dalili za ugonjwa huo hatari, imeongeza Wieara ya Afya katika taarifa.

Televisheni ya Algeria imebaini kwamba mgonjwa aliwekwa karantini katika kituo kimoja jijini Algiers. Lakini mazingira ya maambukizi ya mgonjwa huyo bado hayajawekwa wazi.

Mamlaka ya Algeria imehakikisha kwamba "imeimarisha zaidi mfumo wa kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo kutoka kwa mgonjwa huyo, na mfumo wa uchunguzi na ufuatiliaji katika vituo vyote vya mpakani.

Wiki iliyopita, ripoti iliyochapishwa na wataalamu kadhaa wa magonjwa ya kuambukia haraka katika jarida la Lancet ilitathmini kwamba kuna hatari bara la Afrika kupata haraka ugonjwa huo hatari.

Kulingana na watafiti, Algeria ni moja wapo ya lango tatu muhimu kwa janga hilo kwenye bara la Afrika, pamoja na Misri na Afrika Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.