Pata taarifa kuu
ALGERIA

Algeria yapiga marufuku ndege za jeshi la Ufaransa kwenye anga yake

Mamlaka nchii Algeria imepiga marufuku ndege za jeshi la Ufaransa kwenye anga ya nchi hiyo. Uamuzi huu unakuja wakati mvutano ukiongezeka kati ya Algiers na Paris. Baada ya Ufaransa kuchukuwa hatua kadhaa kuhusiana na visa kwa raia wa Algeria, nchi hizi mbili zinajikuta katika katika sntofahamu.

Ndege za kijeshi za Ufaransa aina ya "Rafale"
Ndege za kijeshi za Ufaransa aina ya "Rafale" AFP PHOTO / ECPAD
Matangazo ya kibiashara

Algeria imefunga anga yake kwa ndege za kijeshi za Ufaransa ambazo kawaida hutumia kwa kuingia au kuondoka katika ukanda wa Sahel ambako wanajeshi wa kikiosi cha Ufaransa cha Operesheni Barkhane wametumwa, msemaji wa makao makuu ya jeshi la Ufaransa.

Jeshi la Ufaransa halijapokea taarifa yoyote rasmi. "Leo (Jumapili) asubuhi, tulsikia tu kwamba Algeria imefunga anga yake kwa ndege za kijeshi za Ufaransa," Kanali Pascal Ianni ameliambia shirika la habari la AFP, akithibitisha habari kutoka Gazeti la kila siku la Figaro. Kulingana na afisa huyo, hata hivyo, "hii haiathiri shughuli au ujumbe wa kijasusi" unaofanywa na Ufaransa huko Sahel.

Makao makuu ya jeshi la Ufaransa yamesema "hawana wasiwasi kufikia sasa". "Ujumbe wa kijasusi wa Ufaransa huko Sahel, uliofanywa kwa njia ya ndege zisizo na rubani, haujaathiriwi pia", amebaini, huku akiongeza kwamba ndege hizi zinafanya kazi zikitokea katika mji wa Niamey, nchini Niger, na hazipiti kwenye anga ya Algeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.