Pata taarifa kuu
ALGERIA-USALAMA

Algeria yafunga anga yake kwa ndege zote kutoka Morocco

Algeria imeamu kufunga anga yake kwa ndege zote za abiria na za kijeshi kutoka Moroco na pia kwa ndege zilizosajiliwa nchini Morocco, ofisi ya rais wa Algeria imetangaza.

Boeing 737 NG / Max ya shirika la ndege la Morocco la Royal Air Maroc.
Boeing 737 NG / Max ya shirika la ndege la Morocco la Royal Air Maroc. PASCAL PAVANI / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Baraza Kuu la Usalama (HCS) limeamua kufunga mara moja anga kwa ndege zote za abiria na za jeshi, ikiwa ni pamoja na zile zilizosajiliwa nchini Morocco", kulingana na taarifa rasmi. Uamuzi huu umetangazwa baada ya mkutano wa HCS na rais Abdelmadjid Tebboune na kutangaza kufuatilia hali hiyo kwenye mipaka na Morocco.

Uamuzi wa kufunga anga ulichukuliwa "kwa kuzingatia kuendelea kwa chokochoko na vitendo vya uhasama kwa upande wa Morocco," imesema taarifa hiyo.

Agosti 24, Algeria ilivunja uhusiano wa kidiplomasia na Morocco, baada ya miezi kadhaa ya mvutano mkali kati ya nchi hizi hasimu za Maghreb. Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ramtane Lamamra wakati huo aliikosoa Rabat kwa "kuendelea na vitendo vya uhasama dhidi ya Algeria". "Idara za usalama na propaganda za Morocco zinafanya vita vya kudhalilisha dhidi ya Algeria, watu wake na viongozi wake," taarifa hiyo imebaini.

Uhusiano kati ya Algeria na jirani yake wa Morocco uliingiliwa na kasoro hivi karibuni kwa sababu, hasa, ya suala tata la Sahara Magharibi.

Kurejeshwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Morocco na Israeli - kwa sababu ya kutambuliwa na Marekani  kwa "uhuru" wa Morocco kuhusu eneo hili - kumezidisha zaidi mvutano na Algeria, inayounga mkono Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.