Pata taarifa kuu

Algeria: Macron atoa wito wa 'kuangalia yaliyopita kwa ujasiri'

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa wito siku ya Ijumaa kchii Algeria kutazama yaliyotokea katika enzi ya ukoloni wa Ufaransa "kwa ujasiri" na kutafuta "ukweli" badala ya "kutubu", katika siku ya pili ya ziara yake rasmi nchini Algeria ambayo tayari imesaidia kuzindua upya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atembelea makaburi ya Ulaya Saint-Eugene huko Algiers, Agosti 26, 2022.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atembelea makaburi ya Ulaya Saint-Eugene huko Algiers, Agosti 26, 2022. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Wakati akitembelea kaburi la Saint-Eugène, kaburi kuu huko Algiers wakati wa ukoloni wa Ufaransa, aliweka shada la maua chini ya mnara wa "waliuawa wakisaidia Ufaransa kupigana", kabla ya jeshi la Ufaransa kuimba mwimbo wa taifa "Marseillaise".

Alipoondoka, Rais wa Ufaransa amejadili mambo mengi mbele ya waandishi wa habari, hasa faili maridadi ya kumbukumbu ambayo ilisababisha ugomvi mkubwa na Algiers.

Baada ya kufufuauhusiano wao siku ya Alhamisi, Bw. Macron na mwenzake, rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune, walitangaza kuundwa kwa tume ya pamoja ya wanahistoria "kuangalia pamoja kipindi hiki cha kihistoria" tangu mwanzo wa ukoloni (1830) hadi mwisho wa Vita vya Uhuru. (1962).

Hii ni mara ya pili kwa Bwana Macron kuzuru Algeria kama rais, baada ya ziara ya kwanza mnamo mwezi Desemba 2017. Mahusiano kati ya nchi hizo mbili wakati huo yalikuwa imara na mkuu wa nchi aliyezaliwa baada ya 1962, ambaye alielezea ukoloni wa Ufaransa kama "uhalifu dhidi ya ubinadamu" kabla ya kuchaguliwa kwake. Lakini uhusiano huo ulisitishwa mara moja, kutokana na kumbukumbu zilizoumiza na miaka 132 ya ukoloni, vita vya umwagaji damu na uchungu wa kuwarejesha nyumbani Wafaransa milioni moja kutoka Algeria.

"Mara nyingi mimi husikia kwamba, juu ya suala la kumbukumbu, tunaitwa kila wakati kuchagua kati ya kiburi na toba. Nataka ukweli, kutambuliwa (kwa sababu) vinginevyo hatutasonga mbele," amesema.

Kwa vijana wa Algeria na vijana wa Kiafrika kwa ujumla, pia ametoa onyo dhidi ya "udanganyifu mkubwa" wa mitandao ya kijamii inayodhibitiwa kwa mbali "chini ya mikono" na mataifa ya kigeni ambayo yanaionyesha Ufaransa kama adui wa nchi yao , akitaja Uturuki, Urusi au China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.