Pata taarifa kuu
HAKI-UFISADI

Algeria: Waziri wa zamani wa nishati ahukumiwa miaka 20 jela

Waziri wa zamani wa Nishati Chakib Khelil, aliyehudumu kwa miaka 10 chini ya utawala wa Abdelaziz Bouteflika, amehukumiwa tena siku ya Alhamisi, akiwa hayupo, kifungo cha miaka 20 jela kwa ufisadi, kulingana na shirika la habari la serikali la APS.

Waziri wa zamani wa Nishati wa Algeria Chakib Khelil.
Waziri wa zamani wa Nishati wa Algeria Chakib Khelil. Wikimedia
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Sidi M'Hamed mjini Algiers pia imewahukumu maafisa wengine wakuu wa zamani vifungo vya kuanzia miaka 5 hadi 10 jela.

Mawaziri hao ni Waziri wa zamani wa Kazi, Amar Ghoul, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Mohamed Bedjaoui, na wakuu wawili wa zamani wa kampuni kubwa ya umma ya hydrocarbon Sonatrach, Noureddine Bouterfa na Abdelmoumen Ould Kaddour.

Walifunguliwa mashtaka kwa "kufuja fedha za umma wakati wa kufunga kandarasi na makampuni ya kigeni". Mahakama pia imethibitisha hati ya kimataifa ya kukamatwa iliyotolewa dhidi ya Bw. Khelil.

Mnamo 2013, vyombo vya sheria vya Algeria vilitoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa Bw. Khelil kama sehemu ya uchunguzi wa malipo ya tume za siri na kampuni tanzu ya kampuni kubwa ya Italia ENI ili kupata kandarasi nchini Algeria, kashfa ambayo imekuwa chini ya kesi kadhaa, nchini Italia na Algeria.

Bw. Khelil aliye kimbilia nchini Marekani, alirejea Algeria mwaka 2016 baada ya mashtaka dhidi yake kuondolewa, kabla ya kurejea nje ya nchi wakati utaratibu ulizinduliwa baada ya kuanguka kwa utawala wa Bouteflika Aprili 2, 2019 chini ya shinikizo la maandamano ya Hirak pamoja na jeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.