Pata taarifa kuu

Morocco na Israel zataka kupanua ushirikiano wao katika 'vita vya kielektroniki'

Morocco na Israel zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wao wa kijeshi kwa kuupanua hadi kwenye ujasusi na usalama wa mtandao, wakati wa mkutano wa ulinzi wa nchi mbili iku ya Jumanne huko Rabat, kulingana na jeshi la Morocco.

Mkuu wa zamani wa jeshi la Israel, Aviv Kochavi Alikwenda Morocco, kwa lengo la kukuza na kuimarisha ushirikiano.
Mkuu wa zamani wa jeshi la Israel, Aviv Kochavi Alikwenda Morocco, kwa lengo la kukuza na kuimarisha ushirikiano. AP - Tsafrir Abayov
Matangazo ya kibiashara

Nchi hizo mbili "zilikubalina kuimarisha zaidi ushirikiano huu na kuupanua katika nyanja zingine, ikiwa ni pamoja na ujasusi, ulinzi wa anga na vita vya kielektroniki," makao makuu ya jeshi la Morocco limesema katika taarifa kwa vyombo vya habari. Tangazo hili linafuatia mkutano wa kwanza wa kamati ya ufuatiliaji wa ushirikiano wa kiulinzi kati ya Morocco na Israel ambao ulifanyika siku ya Jumatatu na Jumanne katika mji mkuu wa Morocco, kama sehemu ya maelewano ya kijeshi kati ya nchi hizo mbili.

Mkutano huo uliongozwa na Inspekta Jenerali wa FAR Belkhir El Farouk na Mkurugenzi wa Ofisi ya Masuala ya Kisiasa na Kijeshi ya Wizara ya Ulinzi ya Israel Dror Shalom. Pande hizo mbili pia zilichunguza vipengele mbalimbali vya ushirikiano wao, ikiwa ni pamoja na "vifaa, mafunzo pamoja na upatikanaji na uboreshaji wa vifaa", inaeleza taarifa kwa vyombo vya habari.

Ushirikiano "unaobeba masilahi ya pande zote mbili na msingi wa kuaminiana na kusaidiana", alikaribisha Belkhir El Farouk, nambari mbili katika jeshi la Morocco. Mnamo mwezi Novemba 2021, Waziri wa Ulinzi wa zamani wa Israeli Benny Gantz alitia saini mkataba wa makubaliano huko Rabat unaosimamia uhusiano wa usalama na Morocco.

Ziara yake ya kihistoria ilifuatiwa mwezi Julai na ile ya mkuu wa zamani wa jeshi Aviv Kochavi, ilikuwa ziara ya kwanza ya mkuu wa majeshi wa Israel katika nchi ya Morocco. Maelewano kati ya Morocco na Israel yameongezeka tangu uhalalishaji wa kidiplomasia uliofanyika mwezi Desemba 2020 ndani ya mfumo wa Makubaliano ya Abraham, mchakato kati ya taifa la Israel na nchi kadhaa za Kiarabu, zinazoungwa mkono na Washington.

Ukaribu huu unatazamwa kwa jicho baya na nchi jirani ya Algeria, inayounga mkono kwa dhati Wapalestina, na hivyo kuzidisha mvutano uliopo kati ya nchi hizo mbili kutokana na kutoelewana kwa kina kuhusu Sahara Magharibi. Mzozo huko Sahara Magharibi unaihusisha Morocco, ambayo inadhibiti 80% ya eneo hilo, dhidi ya wanaharakati wanaotaka kujitenga Polisario wanayoungwa mkono na Algeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.