Pata taarifa kuu

Algeria yatangaza uzinduzi wa mazoezi ya kijeshi ya baharini na Urusi

Mazoezi hayo ya kijeshi na Moscow yatadumu kwa siku nne na yatafanyika katika Bahari ya Mediterania. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Wizara ya Ulinzi ya Algeria inathibitisha kwamba kundi la meli za kijeshi za Urusi zimetua Algeria bila kutaja mahali. Mazoezi haya yanafanywa ndani ya mfumo wa ushirikiano wa kijeshi kati ya vikosi vya nchi hizo mbili, wizara hiyo inaongeza. Algeria inadumisha uhusiano wa ndani na wa kimkakati na Urusi, hasa katika sekta ya kijeshi.

Wanajeshi wa Algeria.
Wanajeshi wa Algeria. REUTERS/Louafi Larbi
Matangazo ya kibiashara

Mazoezi yanayofanyika hivi sasa katika Bahari ya Mediterania ni hatua moja tu katika mfululizo mrefu wa mazoezi ya pamoja ya kijeshi yaliyozinduliwa mwaka 2017 kati ya Algiers na Moscow. Tangu wakati huo, muunganiko mkubwa kati ya majeshi ya Algeria na Urusi umeendelea kusonga mbele, hasa katika suala la mwingiliano.

Mazoezi mengine ya kijeshi yatafanyika mwezi wa Novemba mwaka huu, katika ardhi ya Algeria, huko Bechar, eneo la jangwa lililo karibu na mpaka wa Morocco. Wanajeshi 80 wa Urusi na Waalgeria wengi watashiriki katika mazoezi hayo, ambayo lengo lake ni kupambana na makundi ya kigaidi katika ukanda wa Sahel.

Baada ya Algeria kwa mara ya kwanza kushiriki katika michezo ya kijeshi iliyoandaliwa na Moscow kila mwaka, sehemu ya mashindano haya ya kijeshi ya Urusi ilifanyika kwa mara ya kwanza, mnamo 2021, nchini Algeria.

Mazoezi haya ya pamoja ya kijeshi yanazidi kuwa muhimu. Mwaka mmoja na nusu uliopita, vikosi maalum vya Algeria vilienda kutoa mafunzo huko Caucasus Kaskazini, hasa huko Dagestan.

Mwezi wa Septemba mwaka huu, karibu wanajeshi 100 wa Algeria walishiriki katika mazoezi ya kijeshi ya Vostok 2022, ambayo yalifanyika mashariki ya mbali nchini Urusi. Mazoezi yaliyohusisha washirika wa karibu wa Kremlin.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.