Pata taarifa kuu

Rais wa zamani Thomas Sankara azikwa mahali alipouawa

Miili ya rais wa zamani wa Burkina Faso Thomas Sankara na wasaidizi wake kumi na wawili waliouawa Oktoba 15, 1987 wakati wa jaribio la mapinduzi ya kijeshi, imezikwa siku ya Alhamisi mahali walipouawa huko Ouagadougou, shirika la habari la AFP limebainisha.

Thomas Sankara aliingia madarakani kupiti mapinduzi ya kijeshi mnamo mwezi Agosti 1983, aliuawa Oktoba 15, 1987 wakati wa mapinduzi yaliyochochewa na naibu wake, Blaise Compaoré.
Thomas Sankara aliingia madarakani kupiti mapinduzi ya kijeshi mnamo mwezi Agosti 1983, aliuawa Oktoba 15, 1987 wakati wa mapinduzi yaliyochochewa na naibu wake, Blaise Compaoré. © AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Matangazo ya kibiashara

Maafisa kadhaa wa serikali, akiwemo Waziri Mkuu Apollinaire Joachimson Kyélem de Tambela, walionekana pamoja na wanafamilia zaidi ya mia moja waliokuja karibu na jeneza kumi na tatu.

Mjane wa Thomas Sankara, Mariam Sankara, na watoto wake wawili, ambao hawakukubali uchaguzi wa mahali pa kifo chake kwa maziko yake, hawakuwepo. Lakini watu wengine wa familia hayati rais walikuwepo. Kwanza, majeneza hayo yalibebwa huku yakifunikwa bendera ya Burkina Faso hadi makaburini nyuma ya sanamu kubwa ya Thomas Sankara iliyosimamishwa katika eneo la mauaji yake.

Thomas Sankara aliingia madarakani kupiti mapinduzi ya kijeshi mnamo mwezi Agosti 1983, aliuawa Oktoba 15, 1987 wakati wa mapinduzi yaliyochochewa na naibu wake, Blaise Compaoré. Siku hiyo, rais wa Burkina Faso alikuwa katika mkutano kwenye makao makuu ya Baraza lake la Kitaifa la Mapinduzi (CNR) wakati kundi la askari walipofika na kumpiga risasi yeye na wenzake.

Miili ya Thomas Sankara na wenzake kumi na wawili ilizikwa kwa mara ya kwanza kwenye makaburi nje kidogo ya mji wa Ouagadougou, Mei 25, 2015 kwa madhumuni ya taratibu za kisheria.

Wakili Benewende Sankara, mwanasheria wa familia ya Sankara, ambaye hana uhusiano wa kifamilia naye, alipongeza "mafanikio makubwa ya kutafuta haki kwa Thomas Sankara na waathiriwa wote wa Oktoba 15, 1987".

"Ni furaha kwa vijana wote kwa sababu ni kama kuzaliwa upya," alifurahi Stanislas Damiba, rais wa Shirika llinalotetea haki ya Matima wa Sankara, mamia ya vijana wa Burkina Faso waliotumwa kwa mafunzo nchini Cuba katika miaka ya 1980 na rais huyo wa zamani.

"Sherehe ya kitaifa na kimataifa ya kuwaenzi wahanga itafanyika Oktoba 15, 2023, kuheshimu kumbukumbu zao", kulingana na serikali.

Baada ya kifo cha Sankara, Blaise Compaoré alisalia madarakani hadi maandamano ya kiraia yaliyomng'atua madarakani mwaka wa 2014. Mwezi Aprili mwaka jana, baada ya kesi iliyodumu kwa miezi sita, mahakama ya kijeshi ya Ouagadougou ilimtia hatiani Bw. Compaoré, anayeishi Côte d'Ivoire, na kumhukumu kifungo cha maisha jela kwa jukumu lake katika mauaji ya Thomas Sankara

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.