Pata taarifa kuu

Rais wa zamani wa Burkina Faso Thomas Sankara atazikwa katika eneo alikouawa

Miili ya rais wa zamani wa Burkina Faso Thomas Sankara na wenzake kumi na wawili waliouawa Oktoba 15, 1987 hivi karibuni itazikwa mahali walipouawa huko Ouagadougou, msemaji wa serikali ya Burkina Faso ametangaza siku ya Ijumaa Februari 3, 2023.

Thomas Sankara aliuawa Oktoba 15, 1987.
Thomas Sankara aliuawa Oktoba 15, 1987. AFP - ALEXANDER JOE
Matangazo ya kibiashara

Mazishi haya yatafanyika "mwezi wa Februari" huko Ouagadougou "kwenye eneo la Kumbukumbu ya Thomas Sankara" lililotengwa mahali alipouawa, msemaji wa serikali na Waziri wa Mawasiliano Jean-Emmanuel Ouédraogo amesema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Amebaini kwamba baada ya kesi ya wauaji wao mnamo 2021-2022, watapaswa kuzikwa "kwa njia ya heshima". Miili ya Thomas Sankara na wenzake kumi na wawili ilizikwa kwa mara ya kwanza kwenye makaburi yanayopatikana nje kidogo ya mji wa Ouagadougou, Mei 25, 2015 kwa madhumuni ya taratibu za kisheria.

Mazishi yao mapya "yatafanyika kulingana na taratibu za kitamaduni za mazishi na kufuatiwa na sherehe za kidini na kijeshi", ameongeza, akibainisha kuwa "sherehe ya kitaifa na kimataifa ya kuwaenzi wahanga hao itaandaliwa mnamo Oktoba 15, 2023, kwa kuheshimu kumbukumbu zao" .

Thomas Sankara ambaye aliingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi mnamo mwezi Agosti 1983, aliuawa Oktoba 15, 1987 wakati wa mapinduzi yaliyochochewa na Blaise Compaore, ambaye alikuwa wakati huo naibu wake. Bw;Compaore alibaki madarakani hadi maandamano ya kiraia ambayo yalisababisha kuanguka kwake mnamo 2014.

Katika kipindi chote cha miaka 27 ya Bw. Compaoré madarakani, kifo cha Thomas Sankara, ambaye alitaka "kuondoa ukoloni mawazo" na kuvuruga utaratibu wa dunia kwa kutetea maskini na wanaokandamizwa, lilikuwa suala la mwiko.

Mwezi Aprili, mahakama ya kijeshi ya Ouagadougou ilimhukumu Bwana Compaoré ambaye hayupo, kifungo cha maisha jela kwa jukumu lake katika mauaji ya Thomas Sankara na wenzake kumi na wawili, kufuatia kesi iliyodumu kwa miezi sita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.