Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-HAKI

Kesi ya mauaji ya Sankara: Diendéré amhusisha Waziri Mkuu wa zamani Zida

Mbele ya mahakama ya kijeshi ya mjini Ouagadougou, Jenerali Gilbert Diendéré alidai kuwa aliandaa mkutano kati ya watu wanaohusika na usalama wa rais Thomas Sankara na Kapteni Blaise Compaoré Oktoba 15, 1987.

Jenerali Diendéré, aliyepatikana na hatia ya mapinduzi yaliyoshindwa mwaka 2015, sasa anashtakiwa katika kesi ya mauaji ya Thomas Sankara. Picha: Ouagadougou, 2017.
Jenerali Diendéré, aliyepatikana na hatia ya mapinduzi yaliyoshindwa mwaka 2015, sasa anashtakiwa katika kesi ya mauaji ya Thomas Sankara. Picha: Ouagadougou, 2017. Photo: Ahmed Ouoba/AFP
Matangazo ya kibiashara

Hyacinthe Kafando, afisa wa ngazi ya chini, hakukubali kwenda kwenye mkutano huu. Saa chache baadaye, askari kutoka kutoka kikosi cha ulinzi wa Blaise Compaoré walimpiga risasi rais Thomas Sankara na wenzake.

Ni vigumu kumsikiliza Hyacinthe Kafando katika suala hili: amekimbia nchi tangu 2015. Na hii, kulingana na Jenerali Diendéré, kwa msaada wa Yacouba Isaac Zida, Waziri Mkuu wa zamani katika kipindi cha mpito.

Tangu washtakiwa kuanza kuhojiwa, jina la Hyacinthe Kafando, limeendelea kutajwa katika kesi hiyo.

Wakati wa uchunguzi wa kesi ya Sankara, jaji alitoa wito wa kumsikiliza Hyacinthe Kafando, ambaye bado alikuwa nchini Burkina Faso. Lakini mkuu wa zamani wa usalama wa Kapteni Blaise Compaoré, wakati huo, hakufika katika ofisi ya jaji. "Mpwa wa Hyacinthe Kafando, mwanajeshi katika jeshi la Burkina Faso wakati huo, alinijulisha kuwa kulikuwa na wito kutoka kwa jaji dhidi ya mjomba wake," Jenerali Gilbert Diendéré aliiambia mahakama.

Kulingana na mkuu wa zamani wa jeshi wakati wa utawala wa Blaise Compaoré, Jenerali Yacouba Isaac Zida, Waziri Mkuu wa wakati huo katika kipindi cha mpito, ndiye ambaye alipendekeza Hyacinthe Kafando asiripoti mahakamani Juni 22, 2015. "Yacouba Isaac Zida alimwagiza Mady Pafadnam kumshawishi Hyacinthe Kafando kuondoka nchini Burkinabè, kwa sababu jaji anayemchunguza kesi hiyo angetaka akamatwe", alibaini Jenerali Diendéré. Hivyo ndivyo Koplo Mady Pafadnam alivyompeleka Hyacinthe Kafando hadi kenywe moja ya mipaka ya Burkina Faso, bila kubainisha ni mpaka upi.

Jenerali Gilbert Diendéré anadai kufunguliwa mashtaka katika kesi hii kwa maagizo kutoka kwa Jenerali Yacouba Isaac Zida, ambaye hata hivyo alikuwa amemuahidi kwamba hatafuatiliwa na mtu yeyote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.