Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-HAKI

Kesi ya mauaji ya Thomas Sankara yaanza kusikilizwa nchini Burkina Faso

Kesi ya kihistoria ya mauaji ya aliyekuwa kiongozi wa Burkina Faso Thomas Sankara miaka 34, iliyoahirishwa toka Oktoba 11 had leo Oktoba 25, inaanza kusikilizwa jijiji Ouagadougou.

Watu wanasubiri kufunguliwa kwa kesi ya washtumiwa wa mauaji ya Thomas Sankara, kesi iliyo iliyoahirishwa hadi Oktoba 25, huko Ouagadougou, Oktoba 11, 2021.
Watu wanasubiri kufunguliwa kwa kesi ya washtumiwa wa mauaji ya Thomas Sankara, kesi iliyo iliyoahirishwa hadi Oktoba 25, huko Ouagadougou, Oktoba 11, 2021. AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Matangazo ya kibiashara

Katika kesi hii, watu 14 wanahusishwa na mauaji ya Thomas Sankara akiwemo Blaise Compaoré, rais wa zamani wa Burkina Faso na aliye kuwa rafiki wa Thomas Sankara, na Hyacinthe Kafando, mkuu wake wa usalama.

Blaise Compaoré anashukiwa kuamuru mauaji hayo na Hyacinthe Kafando ndiye aliyetekeleza mauaji hayo. Miaka thelathini na nne baada ya tukio hilo, ufunguzi wa kesi hii ni wa kihistoria. Iliahirishwa baada ya ufunguzi wake kwa mara ya kwanza, itaendelea Jumatatu hii.

Hata hivyo familia ya Sankara inasema, kesi hiyo ni muhimu na hatimaye ukweli utawekwa wazi kuhusu mauaji ya mpendwa wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.