Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-HAKI

Kesi ya Thomas Sankara kufunguliwa Jumatatu hii

Kesi ya kihistoria mauaji ya aliyekuwa kiongozi wa mapinduzi nchini Burkina Faso Thomas Sankara mwaka 1987, inaanza kusikilizwa leo Jumatatu mjini Ouagadougou chini ya ulinzi mkali katika Mahakama ya kijeshi.

Thomas Sankara, kiongozi wa mapinduzi ya Burkina Faso, ambaye alichukua madaraka katika mapinduzi mnamo 1983, aliuawa pamoja na washirika wake 12 mnamo Oktoba 15, 1987.
Thomas Sankara, kiongozi wa mapinduzi ya Burkina Faso, ambaye alichukua madaraka katika mapinduzi mnamo 1983, aliuawa pamoja na washirika wake 12 mnamo Oktoba 15, 1987. © AFP/Dominique Faget
Matangazo ya kibiashara

Usalama umeimarishwa katika jengo la mahakama kuu ya kijeshi katika mji wa Ouagadougou ambapo watu kumi na wanne miongoni mwao rais wa zamani wa Burkina Faso Blaise Compaore, wanatarajiwa  kutoa ushahidi kuhusu namna mauaji ya kiongozi huyo  alivyouawa miaka 34 iliyopita.

Hata hivyo rais wa zamani wa Burkina Faso Blaise Compaore ambaye ametajwa moja kwa moja, kama mshukiwa wa kwanza wa mauaji hayo  atasusia kesi hiyo kwa mujibu wa mawakili wake.

Katika mahojiano maalum na RFI mwandishi mwenzetu Christophe Boibouvier alimuuliza mjane wa Thomas Sankara Bi Mariam Sankara kuhusu kutoonekana mahakamani kwa Blaise Comparee, Bi Mariam amesema na kujiuliza hadi lini Blaise Compaore atakwepa mahakama.

Kepteni Thomas Sankara aliuawa mwaka wa 1987, na wananchi wa taifa hilo la Afrika Magharibi wanatumai kwamba kesi hiyo itatoa mwanga kuhusu mauaji hayo yaliyofuatiwa na kipindi kirefu cha  umwagikaji damu.

Kesi hii iliyosubiriwa kwa miaka mingi, itafuatiliwa nje na ndani ya nchi ya Burkina Faso.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.