Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-HAKI

ECHR yasitisha hatua ya kumsafirisha François Compaoré kwenda Burkina Faso

Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu (ECHR) imesitisha kwa muda, Ijumaa hii, Agosti 6, 2021, kurudishwa kwa François Compaoré kutoka Ufaransa kwenda Burkina Faso. Ndugu wa rais wa zamani Blaise Compaoré anahusika katika kesi ya mauaji ya mwandishi wa habari wa uchunguzi Norbert Zongo, mwaka 1998.

François Compaoré, kaka wa rais wa zamani wa Burkina Faso, Blaise Compaoré (picha ya kumbukumbu).
François Compaoré, kaka wa rais wa zamani wa Burkina Faso, Blaise Compaoré (picha ya kumbukumbu). Ahmed OUOBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

ECHR, ilipokea malalamiko kutoka kwa mawakili wa washtakiwa, inabainisha kuwa ni hatua ya mudao, wakati inachunguza kesi hiyo.

Katika taarifa fupi kwa waandishi wa habari, Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu inaelezea kuwa aina hii ya hatua ya muda inatumika tu wakati kuna "hatari ya karibu ya uharibifu usioweza kurekebishwa", lakini kwamba haitoi maamuzi yake ya baadaye kwa undani zaidi kuhusiana na kesi hii.

Uamuzi huo kwa vyovyote ni wa lazima, kulingana na wanasheria waliyohojiwa na RFI: Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu imesitisha kwa muda agizo la kumsafirisha François Compaoré kwenda Burkina Faso, ambalo awali lilisainiwa Machi 2020 na Waziri Mkuu wa zamani wa Ufaransa Édouard Philippe.

Tangu wakati huo, upande wa utetezi wa kaka wa rais wa zamani wa Burkina Faso ulikuwa umekata rufaa nchini Ufaransa, ukibaini kwamba mteja wake atafanyiwa mateso na madhila mbalimbali huko Ouagadougou.

Lakini kuna uwezekano kuwa uamuzi wa kumsafirisha François Compaoré kwenda Burkina Faso unaweza kucheleweshwa kwa miezi kadhaa, au miaka kadhaa, amebaini mwanasheria wake wakili Pierre-Olivier Sur.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.