Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SHERIA

Mawakili wa Guillaume Soro waahidi kuchukua hatua mpya dhidi ya serikali ya Ivory Coast

Siku mbili baada ya mahakama ya Abidjan nchini Ivory Coast kumhukumu kifungo cha maisha jela aliyekuwa waziri mkuu huyo wa zamani wa nchi hiyo, Guillaume Soro; mawakili wake wamesema kuwa wamejipanga kuchukua hatua zaidi kupinga uamuzi huo.

Mahakama hiyo iliiamuru Cote d'Ivoire isimamishe hati yake ya kukamatwa kwa Guillaume Soro na kuwaachilia ndugu zake 19 ambao walikuwa wamefungwa kwa miezi kadhaa.
Mahakama hiyo iliiamuru Cote d'Ivoire isimamishe hati yake ya kukamatwa kwa Guillaume Soro na kuwaachilia ndugu zake 19 ambao walikuwa wamefungwa kwa miezi kadhaa. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Soro alipatikana na hatia ya makosa ya uhaini na pia kuhatarisha usalama wake rais wa nchi hiyo, huku majaji wa kwenye mahakama ya jijini Abidjan wakimshutumu kwa kueneza taarifa za uongo.

Taarifa ya hukumu ya kifungo cha maisha jela dhidi ya Guillaume Soro ilitolewa akiwa hayupo mahakamani, nchini Ivory Coast.

Wakili wake Affoussiata Bamba Lamine, mkurugenzi wa ofisi yake Soûl tu Soul, pamoja na mbunge wa zamani wa nchi hiyo Ben Souk, kwa upande wao, wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela, na wengine miezi 17.

Guillaume Soro ambaye wakati mmoja alikuwa mshirika wa rais Allasane Outtara ,anatuhumiwa kuhusika kwenye njama ya kijeshi ya kufanya mapinduzi mwaka 2019, miezi kadhaa kabla uchaguzi wa urais nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.