Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SORO-SIASA-HAKI

Guillaume Soro akabiliwa na mashitaka nchini Ufaransa, kwa 'mauaji' na 'uhalifu wa kivita'

Mashitaka ya "mateso, mauaji na uhalifu wa kivita" dhidi ya spika wa zamani wa bunge Guillaume Soro yamewasilishwa mahakamani Alhamisi wiki hii na mawakili 6 wa walalamikaji.

Guillaume Soro wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika makazi yake huko Abidjan, Februari 15, 2019.
Guillaume Soro wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika makazi yake huko Abidjan, Februari 15, 2019. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mawakili hao, Guillaume Soro anashtumiwa makosa hayo yaliyotekelezwa katika mwaka 2003 na 2011 alipokuwa kiongozi wa waasi.

Walalamikaji, raia kutoka Cote d'Ivoire na Ufaransa, wanadai kwamba mpinzani huyo aliye uhamishoni sasa nchini Ufaransa "aliamuru mauaji ya watu 5" wakati wa kitendo kilicholenga kuimarisha uongozi wake kundi la waasi. Mashitaka mawili yamewekwa katika mashitaka hayo.

Binti wa IB. Ibrahim Coulibaly, aliyeuawa Aprili 27, 2011 huko Abidjan, wiki mbili baada ya ushindi wa kambi ya Ouattara ni miongoni mwa watu hao waliouawa.

Wakati huo Guillaume soro, afisa wa cheo cha juu cha Jenerali, aliyejitangaza, maarufu na mwenye kupendwa na watu wengi nchini Cote d'Ivoire, alishiriki katika vita vya kuangusha utawala wa Laurent Gbagbo.

Kwa upande wa mawakili wa walalamikaji, waasi wa kundi la FRCI ndio waliomkamata na kisha kutelekeza maiti yake katikati ya barabara kwa amri ya kiongozi wao Guillaume Soro.

Guillaume Soro pia anashtumiwa kaka wa I. Ibrahim Coulibaly, Soualio Coulibaly na Issiaka Timité, Kassoum Bamba na Abdoulaye Doumbia.

Kassoum Bamba na Abdoulaye Doumbia marafiki wawili wa IB. waliuawa mnamo mwaka 2004, kwa mujibu wa mawakili hao.

Hivi karibuni Mahakama ya Abidjan ilimhukumu Guillaume soro kifungo cha miaka 20 jela kwa kujaribu kuhatarisha usalama wa taifa.

Bw. Soro alitangaza kuwania katika uchaguzi wa urais nchini Cote'Ivoire ambao umepangwa kufanyika mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.