Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-USALAMA

Mauaji Burkina Faso: Serikali yatangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa

Nchini Burkina Faso, watu 47 wameuawa baada ya kutokea kwa shambulizi ya kijihadi Kaskazini mwa nchi hiyo. Thelathini ni raia wa kawaida huku 14 wakiwa ni maafisa wa usalama.

Jjeshi likifanya doria huko Dori, Burkina Faso (picha ya kumbukumbu).
Jjeshi likifanya doria huko Dori, Burkina Faso (picha ya kumbukumbu). © OLYMPIA DE MAISMONT AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Mauaji hayo yametokea kwenye mji wa Gorgadji na rais Roch Marc Christian Kaboré ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.

Serikali nchin humo inasema pamoja na mauaji hayo, maafisa wa usalama walifanikiwa kuwaangamiza magaidi 58 na kuwajeruhi wengine kwenye makabiliano makali.

Shambulizi hilo lilitokea Jumatano mchana baada ya watu wenye silaha kuwashambulia watu kwenye mji wa Boukouma, lakini pia kutekeleza shambulizi la kushtukiza kwa maafisa wa usalama.

Hili ni shambulizi la tatu dhidi ya wanajeshi wa Burkina Faso ndani ya wiki mbili zilizopita, mara ya mwisho ilikuwa ni tarehe 4 mwezi huu wakati walipowauwa wanajeshi na raia 30 karibu na nchi ya Niger.

Burkina Faso, pamoja na mataifa jirani ya Afrika Magharibi ya Niger na Mali, yameendelea kusumbuliwa na wapiganaji wa kijihadi katika êneo hilo la Sahel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.