Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-USALAMA

Burkina Faso: Angalau raia 47 na wanajeshi wauawa katika shambulio Sahel

Karibu raia 30 na askari 14 wameuawa katika shambulio la msafara kati ya eneo mji wa Dori na Arbinda nchini Burkina Faso. Watu ambao walikuwa wakiondoka katika mji wa Dori kuelekea mji wa Arbinda kwenye umbali wa kilomita mia moja wamelengwa na shambulio hilo jipya

Vikosi vya usalama na ulinzi vya Burkinabè vikifanya doria kwenye pikipiki (Picha ya kumbukumbu).
Vikosi vya usalama na ulinzi vya Burkinabè vikifanya doria kwenye pikipiki (Picha ya kumbukumbu). © MICHELE CATTANI/AFP
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya ulinzi na raia wanaojitolea kwa ulinzi wa taifa walifanikiwa kuangamiza magaidi 58 kulingana na chanzo cha usalama. Rais Roch Marc Christian Kaboré ametangaza maombolezo ya kitaifa ya saa 72 kuanzia Alhamisi hii.

Kutokana na  hali ya ukosefu wa usalama katika mkoa wa Sahel, raia wanaotaka kufanya safari kati ya miiji miwili ya Arbinda na Dori, karibu kilomita 100, hawatumii barabara peke yao, wanasindikizwa na vikosi vya usalama. Wafanyabiashara ambao walikuwa wamesindikizwa na askari kutoka Dori kwenda Arbinda walijikuta wakishambuliwa na watu wenye silaha. Askari na raia wanaojitolea kwa ulinzi wa taifa walikuwa wakilinda usalama wa raia hao, kulingana na chanzo rasmi.

Shambulio hilo lilitokea katika kijiji cha Boukouma kilomita 25 kutoka eneo la Gorgadji.

Wanajeshi kumi na wanne na raia wanaojitolea watatu wauawa

Raia thelathini waliuawa.Wanajeshi 14 na raia wanaojitolea 3 kwa kwa ulinzi wa taifa pia wameuawa katika shambulio hilo kulingana na uduru rasmi. Watu 30 walijeuhiwa, na majeruhi mahututi walisafirishwa hadi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Ouagadougou, kulingana na vyanzo vyetu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.