Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-HAKI

Burkina Faso: Kesi ya Thomas Sankara kusikilizwa Oktoba 11, 2021

Mahakama ya kijeshi ya Ouagadougou imetangaza kwamba kesi ya hayati rais wa Burkina Faso Thomas Sankara itafunguliwa Oktoba 11, 2021.

Thomas Sankara, baba wa mapinduzi ya Burkina Faso aliuawa Oktoba 15, 1987 katika jaribio la mapinduzi lililomuweka madarakani Kapteni Blaise Compaoré.
Thomas Sankara, baba wa mapinduzi ya Burkina Faso aliuawa Oktoba 15, 1987 katika jaribio la mapinduzi lililomuweka madarakani Kapteni Blaise Compaoré. William F. Campbell/Time & Life Pictures/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Baba wa mapinduzi ya Burkina Faso aliuawa Oktoba 15, 1987 katika jaribio la mapinduzi lililomuweka madarakani Kapteni Blaise Compaoré.

Blaise Compaoré na wengine kadhaa wanashtakiwa katika kesi hii. Ilichukua miaka 34 kwa siku hiyo iliyosubiriwa kwa muda mrefu kufika, kulingana na mmoja wa mawakili wa familia ya wahanga.

Kulingana na wakili Guy Hervé Kam, mmoja wa mawakili wa familia za wahanga, kufunguliwa kwa kesi hii sio ushindi tu bali pia kwa upande wa familia, ni "wakati wa kujuwa ukweli kuhusiana na tukio hilo". "Imekuwa ni muda mrefu tukisubiri siku hiyo ifikeili  kila mmoja awajibishwe kwa kile alichokifanya Oktoba 15, 1987," amesema wakili huyo.

Ukurasa muhimu katika historia ya Burkina Faso

Wakili Guy Hervé Kam amebaini kwamba kufunguliwa kwa kesi hii ni ukurasa muhimu katika historia ya demokrasia nchini Burkina Faso na kwa familia za wahanga.

Kwa jumla, watu 14 watajibu mashataka yanayowakabili. Rais wa zamani Blaise Compaoré aliye uhamishoni nchini Côte d’Ivoire ambaye hati ya kukamatwa imetolewa dhidi yake ni miongoni mwa watu hao. Anashtakiwa kwa kosa la kuhatarisha usalama wa taifa, kuhusika katika mauaji na kuficha maiti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.