Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-ZONGO-HAKI

Kesi ya Norbert Zongo: François Compaoré hataki kuhukumiwa Burkina Faso

Kaka wa aliekua rais wa Burkina Faso Blaise Compaore ameiambia Mahakama ya Rufaa ya Paris, nchini Ufaransa, kwamba hataki kuhukumiwa nchini Burkina Faso.

François Compaoré, kaka wa aliekua rais wa Burkina Faso Blaise Compaoré, akiiingiza kadi yake katika sanduku la kupigia kura  Ouagadougou, Desemba 2, 2012 (picha ya zamani).
François Compaoré, kaka wa aliekua rais wa Burkina Faso Blaise Compaoré, akiiingiza kadi yake katika sanduku la kupigia kura Ouagadougou, Desemba 2, 2012 (picha ya zamani). FP PHOTO / AHMED OUOBA
Matangazo ya kibiashara

Kesi yake imeahirishwa hadi Machi 7, Wizara ya Sheria ya Burkina Faso imetangaza katika taarifa yake.

François Compaoré, aliefanyiwa uchunguzi kuhusu mauaji ya mwandishi wa habari Norbert Zongo, alieuawa mnamo mwaka 1998, alikamatwa katika uwanja wa Charles de Gaulle jijini Paris mwishoni mwa mwezi Oktoba.

Burkina Faso imekua ikiomba mtuhumiwa huyo arejeshwe nchini humo ajibu tuhuma zinazomkabili.

Waziri wa Sheria nchini wa Burkina Faso, René Bagoro, ameviambia vyombo vya habari kwamba tayari barua imeandikwa kuelekea nchini Ufaransa kuwaomba viongozi wa Ufaransa kumrejesha mtuhumiwa huyo ili ahukumiwe nyumbani.

Wakili wa François Compaoré, Pierre Olivier amesema kwa sasa mteja wake yupo huru licha ya kwamba hawezi kuondoka nchini Ufaransa, wanachosubiri ni serikali ya Burkinafaso kueleza anarejeshwa nchini humo kwa misingi gani.

François Compaoré, kaka wa rais wa zamani wa Burkina Faso Blaise Compaoré, alikamatwa mnamo Octoba 29 katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle jijini Paris, kwa mujibu wa wakili wake, Pierre-Olivier Sur Sur.

Hati ya kimataifa ya kukamatwa ilitolewa na mahakama ya Burkina Faso kuhusiana na uchunguzi juu ya mauaji ya mwandishi wa habari Norbert Zongo mwaka 1998.

Mwili wa mwandishi wa habari Norbert Zongo na wenzake watatu ulikutwa umechomwa moto ndani ya gari mnamo mwezi Desemba mwaka 1998 wakati alikuwa akifanya uchunguzi kuhusu kifo cha David Ouedraogo, dereva wa François Compaoré.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.