Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-ZONGO-HAKI

Kaka wa Blaise Compaoré akamatwa Ufaransa

François Compaoré, kaka wa rais wa zamani wa Burkina Faso Blaise Compaoré, alikamatwa siku ya Jumapili asubuhi Octoba 29 katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle jijini Paris, kwa mujibu wa wakili wake, Pierre-Olivier Sur Sur.

François Compaoré, ndugu wa Blaise Compaoré, hapa ilikua mwaka 2012 Ouagadougou.
François Compaoré, ndugu wa Blaise Compaoré, hapa ilikua mwaka 2012 Ouagadougou. AFP PHOTO / Ahmed OUOBA
Matangazo ya kibiashara

Hati ya kimataifa ya kukamatwa ilitolewa na mahakama ya Burkina Faso kuhusiana na uchunguzi juu ya mauaji ya mwandishi wa habari Norbert Zongo mwaka 1998.

Mara kadhaa alifanya safari kati ya Cote d' Ivoire na Ufaransa ambapo anaishi mke wake na watoto zake watatu , na hivi karibuni alisema katika mahojiano na gazeti la Jeune Afrique kwamba hana hofu na hati ya kukamatwa iliyotolewa dhidi yake Mei 5 mwaka huu. François Compaoré alikamatwa na polisi wa Ufaransa siku ya Jumapili asubuhi aliporudi kutoka Abidjan katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle mjini Paris.

Jaji anatafakari kuhusu uamuzi wa kumuachia huru François Compaore ambaye kwa sasa yuko chini ya udhibiti wa polisi ya mipaka. Utaratibu unaweza kuchukua masaa 48. Akihojiwa na RFI, Pierre-Olivier Sur, mwanasheria wake, alisem akuwa anaamini kwamba mteja wake alikamatwa kwa sababu za "kisiasa".

"Itachukua masaa machache. Utaratibu unatoa saa 48 kabla ya kuwasilishwa kwa ofisi kuu yamashitaka, lakini tunatarajia kwamba, ataachiwa huru na kisha sisi, wanasheria wake, tutakuwa na fursa na kupata nafasi ya kulaani mambo hayo ya kisiasa, "Pierre-Olivier Sur amesema.

Katika Ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa Burkina Faso, mjini Ouagadougou, wamekaribisha hatua hii ya kukamatwa kwa Francois Compaore, kufuatia hati ya kimataifa y kukamatwa kwake iliyotolewa na Burkina Faso.

Wakati huo huo, msemaji Serikali ya Burkina Faso amehakikishia RFI kuwa nchi yake itaomba Francois Compaore asafirishwe mjini Ouagadougou.

Mwili wa mwandishi wa habari Norbert Zongo na wenzake watatu ulikutwa umechomwa moto ndani ya gari mnamo mwezi Desemba mwaka 1998 wakati alikuwa akifanya uchunguzi kuhusu kifo cha David Ouedraogo, dereva wa Francois Compaore.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.