Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-HAKI

Burkina Faso: kesi ya washtakiwa wa mauaji ya Sankara yaahirishwa hadi Oktoba 25

Kesi ya watu wanaodaiwa kuhusika katika mauaji, wakati wa mapinduzi ya serikali ya mwaka 1987, ya mwanamapinduzi wa Burkina Faso Thomas Sankara, wakati huo rais wa nchi hiyo mwenye umri wa miaka 37, imeahirishwa Jumatatu hii hadi Oktoba 25, kwa ombi la mawakili wawili wa upande wa utetezi, ambao wameomba muda zaidi wa kuandaa utetezi wao.

Mara tu baada ya kufunguliwa Jumatatu, Oktoba 11, 2021, kesi ya mauaji ya Thomas Sankara imeahirishwa hadi Oktoba 25 ili kuruhusu mawakili wa upande wa utetezi kujiandaa.
Mara tu baada ya kufunguliwa Jumatatu, Oktoba 11, 2021, kesi ya mauaji ya Thomas Sankara imeahirishwa hadi Oktoba 25 ili kuruhusu mawakili wa upande wa utetezi kujiandaa. AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Matangazo ya kibiashara

Mara tu baada ya kufunguliwa Jumatatu hii, Oktoba 11, kesi ya mauaji ya 1987 ya "baba wa mapinduzi wa Burkina Faso", Thomas Sankara, imeahirishwa hadi Oktoba 25 saa 9 asubuhi. Mkuu wa mahakama ya kijeshi ya mjini Ouagadougou, Urbain Méda, amekubali ombi kutoka kwa mawakili wawili wa upande wa utetezi, ambao waliona hawakuwa na muda wa kutosha kusoma "hati 20,000 kuhusiana na kesi hiyo". Walikuwa wameomba kuahirishwa kwa mwezi mmoja, ili kuweza  "kudhihirisha ukweli". Walipewa wiki mbili, wakati mji mkuu kwa sasa uko chini ya ulinzi mkali kwa wakati huu muhimu.

Watu 14 akiwemo rais wa zamani Blaise Compaore wanashtumiwa kuhusika na mauaji ya kiongozi huyo aliyekuwa na ushawishi mkubwa na alieondolewa madarakani na Compaore katika mapinduzi ya mwaka 1987.

Mjane wa Rais Sankara, Mariam, ambaye hivi karibuni alifanya mahojiano na RFI, alikuwepo wakati wa ufnguzi wa kesi hiyo. "Ni siku ya ukweli kwangu, kwa familia yangu na raia wote wa Burkina Faso", alitangaza mapema asubuhi. Atalazimika kusubiri kwa muda mrefu kidogo. Kwa upande mwingine, mshtakiwa mkuu, rais wa zamani wa Burkina Faso Blaise Compaoré, 70, hakuripoti mahakamani. Blaise Compaoré, rafiki wa karibu na waziri wa Thomas Sankara, alieindia madarakani mwaka 1987 na kupinduliwa mnamo 2014, anaishi nchini Côte d'Ivoire.

Mjane wa Rais Sankara, Mariam, ambaye hivi karibuni alifanya mahojiano na RFI, alikuwepo wakati wa ufnguzi wa kesi hiyo.
Mjane wa Rais Sankara, Mariam, ambaye hivi karibuni alifanya mahojiano na RFI, alikuwepo wakati wa ufnguzi wa kesi hiyo. AFP - OLYMPIA DE MAISMONT

Washtakiwa kumi na wawili kati ya kumi na wanne walikuwa mahakamani wakati wa ufunguzi wa kesi hiyo.

Gilbert Diendéré, aliyeonekana akiwa kizimbani, wakati wa ufunguzi wa kesi ya wauaji wa Thomas Sankara.
Gilbert Diendéré, aliyeonekana akiwa kizimbani, wakati wa ufunguzi wa kesi ya wauaji wa Thomas Sankara. AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.