Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-USALAMA

Wanajeshi 14 wauawa katika shambulio Kaskazini mwa Burkina Faso

Angalau wanajeshi 12 waliuawa katika shambulio Jumatatu wiki hii, kulingana na vyanzo vya usalama. Kikosi cha kijeshi cha Yirgou, kilichoko katika mkoa wa Barsalogho katika jimbo la Kaskazini, kililengwa na watu wenye silaha.

Wanajeshi wa Burkina Faso wakiwa kwenye mazoezi na jeshi la Ufaransa kaskazini mwa Burkina Faso, Novemba 2019.
Wanajeshi wa Burkina Faso wakiwa kwenye mazoezi na jeshi la Ufaransa kaskazini mwa Burkina Faso, Novemba 2019. © AFP/Michele Cattani
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo vetu shambulio hilo la watu wenye silaha lilitokea mapema Jumatatu asubuhina lililenga kikosi cha jeshi la Yirgou. Kulingana na Wizara ya Ulinzi, lilikuwa shambulio la kigaidi ambalo liliwalenga wanajeshi wa Burkina Faso. "Kwa kukabiliana na washambuliaji ambao walikuja kwa wingi na wakiwa na silaha kali za kivita, wanajeshi wa Burkina Faso walipambana vilivyo na kuwaangamiza watu hao," amesema Waziri wa Ulinzi.

Washambuliaji hao wanasemekana kuja na pikipiki na magari madogo. Kufuatia urushianaji huo wa risasi, angalau askari kumi na wanne waliuawa, na wengine kadhaa walijeruhia. Wote waliojeruhiwa walisafirishwa kwenda katika mji wa Foubé, ulioko karibu kilomita sitini kaskazini mwa mji wa Barsalogho, kwa kuendelea kupewa huduma.

"Vifaa vingi vya kijeshi vilipelekwa na wauaji" mali ya jeshi lilichukuliwa na washambuliaji, huficha, chanzo cha usalama kimebaini bila kutoa maelezo zaidi. Chanzo kingine kinasema kuwa magari manne ya kijeshi, gari la wagonjwa, pikipiki, silaha za pamoja na risasi vilichukuliwa na washambuliaji hao. Pia walichoma gari ya kijeshi aina ya Cobra na vifaa kabla ya kuondoka kwenye kambi hiyo, kulingana na vyanzo vyetu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.