Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-USALAMA

Shambulio Burkina: Idadi ya vifo yaongezeka hadi 80, ikiwa ni pamoja na raia 65

Watu themanini - raia 65 na askari 15 - waliuawa katika shambulio la wanajihadi siku ya Jumatano dhidi ya msafara wa kijeshi uliokuwa ukiwasindikiza raia kaskazini mwa Burkina Faso, kulingana na ripoti mpya rasmi iliyotolewa Alhamisi jioni.

Askari wa Burkina Faso huko Ouagadougou (picha ya kumbukumbu).
Askari wa Burkina Faso huko Ouagadougou (picha ya kumbukumbu). AFP PHOTO / SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

"Kulingana na ripoti mpya iliyotolewa leo saa 12:50 jioni (saa za eneo Burkina Faso), raia 65 waliuawa katika shambulio hili la kigaidi," ilisema taarifa kutoka kwa Waziri wa Mawasiliano na msemaji wa serikali, Ousséni Tamboura.Mapema kidogo, chanzo cha serikali kilikuwa kimetangaza askari 14 waliouawa, baada ya kifo cha askari wa 15 aliyefariki kutokana na majeraha aliyoyapata, habari ambayo ilithibitishwa na polisi Alhamisi jioni.

Raia 65 waliouawa ni wanaume 52, wanawake saba na watu sita kutoka kundi la wanamgambo wanaojitolea kwa ulinzi wa taifa (VDP). Watu Sitini na nne walizikwa Alhamisi huko Arbinda, katika mkoa wa Sahel (kaskazini) ambapo shambulio hilo lilitokea.

"Serikali imerudi kutoa rambirambi kwa familia zilizofiwa na inawapongeza vikosivya wa ulinzi na usalama na kundila wanamgambo la VDP kwa hatua yao ambayo imewezesha kuangamiza magaidi zaidi ya 58 kulingana na hesabu ya mwisho," ilisema taarifa hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.