Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-HAKI

Burkina Faso: Rais wa zamani Blaise Compaoré ahukumiwa kifungo cha maisha

Rais wa zamani wa Burkina Faso, Blaise Compaoré, amehukumiwa Jumatano kifungo cha maisha jela kwa kushiriki katika mauaji ya mtangulizi wake Thomas Sankara, aliyeuawa pamoja na wasaidizi wake kumi na wawili wakati wa mapinduzi ya maka 1987.

Blaise Compaoré (kwenye picha), ambaye yuko uhamishoni tangu mwaka 2014 nchini Côte d'Ivoire, na Hyacinthe Kafando ambaye yuko mafichoni tangu mwaka 2016, hawakuhudhuria kesi hii iliyoanza miezi sita iliyopita.
Blaise Compaoré (kwenye picha), ambaye yuko uhamishoni tangu mwaka 2014 nchini Côte d'Ivoire, na Hyacinthe Kafando ambaye yuko mafichoni tangu mwaka 2016, hawakuhudhuria kesi hii iliyoanza miezi sita iliyopita. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya kijeshi ya Ouagadougou pia imehukumiwa kifungo cha maisha jela kamanda wa kikosi chake cha ulinzi Hyacinthe Kafando na Jenerali Gilbert Diendéré, mmoja wa viongozi wa jeshi wakati wa mapinduzi ya mwaka 1987.

Blaise Compaoré, ambaye yuko uhamishoni tangu mwaka 2014 nchini Côte d'Ivoire, na Hyacinthe Kafando ambaye yuko mafichoni tangu mwaka 2016, hawakuhudhuria kesi hii iliyoanza miezi sita iliyopita.

Ilichukua miaka kadhaa ya uchunguzi, kesi ambayo walihusishwa mashahidi zaidi ya 110 na kesi hii imesikilizwa kwa miezi 6 ya hadi leo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.