Pata taarifa kuu

Benin: Ajali mbaya ya barabarani yaua watu wasiopungua ishirini

Magari mawili, basi na lori, ziligongana siku ya Jumapili hii, Januari 29 katikati mwa nchi na kuua watu kadhaa. Ripoti ya mwisho imebaini watu 20 walifariki na 22 waliojeruhiwa ambao walipelekwa hadi hospitalini, hii ikiwa ni ripoti ya awali. Hii ni moja ya ajali mbaya zaidi za barabarani nchini Benin katika miaka ya hivi karibuni.

Moja ya barabara za Benin.
Moja ya barabara za Benin. RFI/Delphine Bousquet
Matangazo ya kibiashara

Ajali hii mbaya ilitokea kwenye lango la kuingilia mji wa Dassa, kilomita 200 kutoka mji wa Cotonou, Jumapili mchana kati ya lori la mizigo na basi. Waliofariki waliangamia kwa moto, waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini wakiwa wameungua vibaya kwa moto, kwani moto ulizuka baada ya ajali hiyo.

Maafisa wa idara ya Zima moto ya Dassa na mji jirani wa Savalou waliingilia kati, walifika eneo la tukio baada ya moto kuzima na kutoa miili ishirini iliyoteketea kwa moto. Waliojeruhiwa walepewa huduma ya mwanzo katika hospitali ya eneo hilo. Baadhi walihamishwa hadi CNHU huko Cotonou.

Patrice Talon aliwatuma Mawaziri wa Mambo ya Ndani na Uchukuzi kwenye eneo la ajali. "Kutakuwa na muendelezo ili hili lisitokee tena," ameandika msemaji wa serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.