Pata taarifa kuu

Chama cha upinzani chakataa matokeo ya uchaguzi wa wabunge nchini Benin

Chama kikuu cha upinzani nchini Benin ambacho kinalaani udanganyifu katika uchaguzi wa wabunge uliyofanyika hivi karibuni, kimekataa matokeo ya muda ya uchaguzi wa wabunge ambao unaipa ushindi kambi ya Rais Patrice Talon.

Bango la chama cha Kidemocrasia "Les Démocrates", kabla ya uchaguzi wa wabunge uliofanyika Benin Januari 8, 2023.
Bango la chama cha Kidemocrasia "Les Démocrates", kabla ya uchaguzi wa wabunge uliofanyika Benin Januari 8, 2023. AFP - YANICK FOLLY
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na matokeo haya, yaliyochapishwa siku moja kabla na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (CENA), muungano wa vyama vinavyounga mkono utawala, umepata viti 81 kati ya 109 bungeni, dhidi ya 28 vya chama kikuu cha upinzani, Democrats. Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutangazwa siku ya Ijumaa.

Uchaguzi huu unaashiria kurejea kwa upinzani bungeni baada ya miaka minne pasina kuwepo kwa chama cha upinzani kutokana na kubanwa kwa kanuni za uchaguzi na mamlaka.

Katika mkutano na waandishi wa habari mapema Alhamisi asubuhi, Kiongozi wa chama cha Democrats Eric Houndete amelaani 'wizi' wa kura na ununuzi wa kura unaofanywa na vyama viwili vikuu vinavyounga mkono mamlaka, lakini ameshindwa kutoa ushahidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.