Pata taarifa kuu

Benin: Upinzani kushiriki katika uchaguzi wa wabunge

Hatimaye upinzani nchini Benin umedhinishwa kushiriki katika uchaguzi wa wabunge wa mwezi Januari 2023, miaka minne baada ya kutengwa kwenyeuchaguzi wa mwisho na baada ya maandamano yaliyokandamizwa.

Rais wa Benin Patrice Talon.
Rais wa Benin Patrice Talon. AFP - PIUS UTOMI EKPEI
Matangazo ya kibiashara

Wikiendi iliyopita, vyama saba vya kisiasa vikiwemo vitatu vinavyodai kuwa vya upinzani viliidhinishwa kushiriki katika uchaguzi wa tarehe 8 Januari. Hapo awali chama kikuu cha upinzani cha The Democrats kilikataliwa kuwania katika uchaguzi, leo kimekubaliwa baada ya uamuzi wa Mahakama ya Katiba.

"Hatujaamini, lakini Mahakama ya Katiba imetaka kuepusha Benin isitumbukiii katika janga jipya kwa kukubali kwamba chama chetu hatimaye kiende kwenye uchaguzi", amesema Gandonou Eudes, kada wa Chama cha The Democrats. Kwa mara ya kwanza, chama kinachompinga Rais Patrice Talon kitashiriki katika uchaguzi.

Uchaguzi uliopita wa wabunge wa 2019 ulimalizika kwa ghasia zilizosababisha vifo vya watu kadhaa, idadi ambayo haijajulikana hadi leo. Upinzani ulipigwa marufuku kushiriki katika uchaguzi huo na wafuasi wake, ambao waliingia mitaani katikati mwa nchi, ngome ya Rais wa zamani Thomas Boni Yayi, walikandamizwa vikali.

Ni vyama viwili tu vya kisiasa vinavyomuunga mkono Rais Patrice Talon ambavyo viliruhusiwa kushiriki katika uchaguzi huu. Mnamo 2021, viongozi wakuu wa upinzani pia hawakushiriki katika uchaguzi wa rais.

Wapinzani wawili wakuu wa rais bado wako gerezani, wamehukumiwa vifungo vikubwa. Ghasia zilizuka tena katikati mwa nchi, huku waandamanaji wakitaka uchaguzi shirikishi ufanyike.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.