Pata taarifa kuu
USALAMA-HAKI

Watu wawili wauawa katika shambulizi kaskazini mwa Benin

Shambulio kwenye kituo cha forodha huko Malanville, kaskazini mashariki mwa Benin, limeua watu wawili. Mamlaka inataka kuwa angalifu kuhusu motisha ya washambuliaji wakati wakisubiri uchunguzi kuhitimishwa.

Katika miezi ya hivi karibuni, mashambulizi ya pikipiki yameongezeka dhidi ya vikosi vya usalama katika sehemu ya kaskazini.
Katika miezi ya hivi karibuni, mashambulizi ya pikipiki yameongezeka dhidi ya vikosi vya usalama katika sehemu ya kaskazini. AFP - YANICK FOLLY
Matangazo ya kibiashara

"Ndio kulikuwa na tukio, lakini hakuna uhakika kuhusu asili ya shambulio". Akihojiwa, Jumatano hii, Septemba 14, kando ya mkutano wa kila wiki wa Baraza la Mawaziri, msemaji wa serikali ya Benin Wilfried Léandre Houngbédji alikataa kubaini ikiwa kitendo hiki ni cha kigaidi au kuhusu shambulio hilo baya lililotokea saa chache baadaye mapema kaskazini mwa Benin.

Watu wenye silaha walishambulia mapema asubuhi katika kituo cha forodha huko Malanville, mji wa mpakani na Niger. Idadi ya waliouawa ni watu wawili, ikiwa ni pamoja na raia waliotambuliwa kama "washiriki wasio rasmi" wa maafisa wa forodha kwenye eneo la tukio.

Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo. Serikali inabaini kwamba "wahalifu waliokuwa kwenye pikipiki wakiwa na silaha ndio kujaribu kushambulia kituo cha forodha kisicho kuwa na ulinzi maalum, tofauti na kituo cha polisi au kitengo cha jeshi".

Wilfried Léandre Houngbédji pia anakataa kuhusisha wanajihadi kwa shambulio bila uchunguzi wa kina.

Katika miezi ya hivi karibuni, mashambulizi ya pikipiki yameongezeka dhidi ya vikosi vya usalama katika sehemu ya kaskazini, huku Rais Patrice Talon akijaribu kusifu nchi hiyo kama kivutio cha kuvutia wawekezaji. Hali ambayo inatia wasiwasi zaidi kwani Benin imeepushwa kwa muda mrefu na tishio la ugaidi ambalo limekuwa hali halisi katika Afrika Magharibi kwa miaka kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.