Pata taarifa kuu
BENIN-USALAMA

Wanajeshi watano waangamia katika shambulio jipya kaskazini-magharibi mwa Benin

Benin ilikumbwa tena Jumatatu na shambulio baya la kigaidi kaskazini magharibi mwa nchi. Hasara ni kubwa, askari watano wa jeshi la ulinzi wa taifa waliuawa. Mwanajeshi mmoja alijeruhiwa vibaya na amepelekwa hospitalini kwa matibabu.

Tanguiéta, mji wanakopitia kwa kuingia katika Hifadhi ya Pendjari nchini Benin.
Tanguiéta, mji wanakopitia kwa kuingia katika Hifadhi ya Pendjari nchini Benin. RFI/Sidy Yansané
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitokea kaskazini magharibi mwa nchi hiyo kwenye mpaka na Burkina Faso, kwa mujibu wa duru zinazofahamu suala hilo, katika eneo la Pendjari ambako makundi ya kigaidi yameshamiri.

Jumatatu asubuhi, wanamgambo wa Kislamu walishambulia kwa vilipuzi vilivyoboreshwa. Shambulio lililoambatana na dhambulio lingine la kuvizia kwa mujibu wa taarifa zetu.

Msafara wa magari yaliyokuwa yakipeleka chakula kwa wanajeshi walio katika maeneo mbalimbali ulikubwa na shambulio la kushtukizaa. Ripoti hiyo inabainiha kuwa wanajeshi watano waliuawa. Miili ya wanajeshi waliouawa imepatikana na kwa mujibu wa chanzo cha usalama, jeshi la Benin bado linashikilia misimamo yake kwa vita.

Tangu shambulio la mwezi Februari, makundi ya kigaidi yenye silaha yameanza kuonyeha nguvu na uwepo wake.

Jumatano ya wiki iliyopita, Rais wa Benin Patrice Talon alimteua Mkuu mpya wa Majeshi. Jenerali Fructueux Gbaguidi, 54, anatarajia kuchukua uongozi wa jeshi leo Jumanne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.