Pata taarifa kuu
BENIN-HAKI

Benin: Joël Aïvo ahukumiwa kifungo cha miaka kumi jela

Mwanasiasa wa upinzani nchini Benin Joël Aivo amehukumiwa na Criet, Mahakama ya Kukandamiza Uhalifu wa Kiuchumi na Ugaidi. Mtaalamu huyo wa masuala ya katiba na washtakiwa wenzake wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka kumi jela. 

Joël Aïvo ni profesa wa sheria ya kikatiba nchini Benin.
Joël Aïvo ni profesa wa sheria ya kikatiba nchini Benin. Joël Aïvo/Archive personnelle
Matangazo ya kibiashara

Washtakiwa wamepatikana na hatia ya utakatishaji fedha na kula njama dhidi ya mamlaka ya serikali. Uamuzi ulitolewa mapema Jumanne hii huko Porto Novo mbele ya hadhara ya watu walioshangaa na waliopigwa na butwaa.

Jaji mkuu alipomuuliza: una nini cha kuongeza katika utetezi wako? Joël Aïvo amejibu, fanya unachotaka kuhusu mimi... Uamuzi huo umetolewa saa nane na nusu usiku wa leo Jumanne: profesa anapokea kifungo cha miaka kumi cha uhalifu; hukumu kama hiyo imepewa kwa washtakiwa wengine wawili, askari wawili. Afisa wake mmoja ameachiliwa kwa kukosa ushahidi.

Mkewe Gladys alimchukua muda mrefu akikumbatiana nae mikononi mwake. Mawakili, wakiwa wamekata tamaa kwa kukosa kuachiliwa kwa mteja wao, walimkaribia wote na kumkumbatia na kumtakia ujasiri. Wakati wa kesi hiyo ikisikilizwa walishutumu ukosefu wa ushahidi na kubaini kwamba kesi iko tupu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.