Pata taarifa kuu
BENIN- SIASA- UCHAGUZI

Benin: Tume ya uchaguzi inasubiriwa kutangaza matokeo ya uchaguzi wa wabunge

Tume ya uchaguzi nchini Benin, imesema imeendelea kupokea karatasi za kupigia kura kutoka kwenye majimbo mbalimbali ya nchi hiyo, na kwamba zoezi la ujumuishaji matokeo linaendelea na huenda hadi kufikia kesho watakuwa wametangaza matokeo rasmi.

Uchaguzi wa wabunge nchini Benin
Uchaguzi wa wabunge nchini Benin AFP - YANICK FOLLY
Matangazo ya kibiashara

Ruffin Domingo, ni mkuu wa operesheni za ulinzi wa kura katika tume ya uchaguzi.

“Tunayafungua kwa sasa maboxi haya na kutoa ripoti ya kura zilizopigwa, baadae tunazikusanya katika chumba cha komputa kupata kanzi data zote.”amesema Ruffin Domingo.

Uchaguzi wa mwishoni mwa juma lililopita, unatarajiwa kuwa kipimo kwa rais Patrice Talon, ambapo kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani, upinzani umeshiriki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.