Pata taarifa kuu
BENIN- SIASA

Benin: Raia wanasubiri matokeo ya uchaguzi wa wabunge

Wananchi wa Benin, wanasubiri matokeo ya uchaguzi wa wabunge, uliofanyika jana, huku idadi ya wapiga kura ikiripotiwa kuwa ndogo.

 Patrice Talon, Rais wa Benin
Patrice Talon, Rais wa Benin AFP - YANICK FOLLY
Matangazo ya kibiashara

Vyama vya upinzani, vilishiriki kwa mara ya kwanza, baada ya kususia uchaguzi wa miaka iliyopita.

Rais Patrice Talon amesema uchaguzi huo  umebadilisha historia ya kisiasa nchini humo.

Daniel Quenum, ni mwangalizi wa uchaguzi huo.

“Nilitarajia kuona idadi kubwa ya watu kama ilivyokuwa mwaka wa 2019 lakini kulikuwa na taharuki jambo ambalo lilitia dosari katika demokrasia.” Amesema Daniel Quenum

Matokeo ya mwisho, yanatarajiwa kuwa wazi kwa siku chache zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.