Benin: Upinzani wapinga matokeo ya uchaguzi wa wabunge
Chama kikuu cha upinzani nchini Benin, kimekataa matokeo ya uchaguzi wa wabunge, ikidai kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na wizi na ununuzi wa kura, ili kukipa ushindi chama cha rais Patrice Talon.
Imechapishwa:
Cheza - 00:33
Kiongozi wa chama cha Demokrasia Eric Houndete, amesema matokeo ya uchaguzi huo, hayakubaliki baada ya Tume ya Uchaguzi kutangaza kuwa kilipata viti 28 huku chama tawala cha rais Talon, kikipata viti 81.
“Chama cha Democrat kinatupilia mbali matokeo ambayo hayakuheshimu maamuzi ya wanachi. ” amesema Eric Houndete.
Vyama vya upinzani viliruhusiwa kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha muda mrefu kushiri katika uchaguzi huo wa wiki hii wa wabunge.