Pata taarifa kuu

Benin: Muungano wa vyama vya siasa unaotawala watangazwa ushindi wa uchaguzi wa wabunge

Mahakama ya Katiba nchini Benin, imethibitisha ushindi wa muungano wa vyama vya siasa unaotawala kama mshindi wa uchaguzi wa wabunge uliofanyika Jumapili, iliyopita.

Matokeo yaliyoidhinishwa yanaonesha kuwa muungano huo uaotawala unaoundwa na vyama viwili vya Progressiste le Renouveau na Bloc Republicain viliibuka mshindi kwa kila chama kupata asilimia 37.56 na 29.23 ya kura.
Matokeo yaliyoidhinishwa yanaonesha kuwa muungano huo uaotawala unaoundwa na vyama viwili vya Progressiste le Renouveau na Bloc Republicain viliibuka mshindi kwa kila chama kupata asilimia 37.56 na 29.23 ya kura. AFP - YANICK FOLLY
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu wa Mahakama huu umekuja siku moja baada ya vyama vya upinzani, vilivyoshiriki kwenye uchaguzi huo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2019 kukataa matokeo hayo na kudai kura zao ziliibiwa. 

Matokeo yaliyoidhinishwa yanaonesha kuwa muungano huo uaotawala unaoundwa na vyama viwili vya Progressiste le Renouveau na Bloc Republicain viliibuka mshindi kwa kila chama kupata asilimia 37.56 na 29.23 ya kura. 

Nacho chama cha rais wa zamani Thomas Boni Yayi, cha Les Démocrates, kimemaliza katika nafasi ya tatu kupata asilimia 24.16 ya kura. 

Vyama vingine vine vilivyosalia, hakuna hata kimoja, kilichopaya asiliia 10 ya kura, katika kinyanganyiro cha kuwania viti 109 vya wabunge nchini humo. 

Demokrasia nchini Benin, imekuwa ikionekana kama mfano katika eneo la Afrika Magahribi, lakini ulianza kutiwa doa baada rais Patrice Talon, kutotimiza ahadi ya kuwania urais kwa muhula wa pili na badala yake kuanza kuwalenga wapinzani. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.