Pata taarifa kuu

Shambulio la Grand Bassam: Washtakiwa wanne wahukumiwa kifungo cha maisha

Mahakama ya Juu ya Abidjan siku ya Jumatano imewahukumu kifungo cha maisha jela washtakiwa wanne wa shambulio la wanajihadi katika mji wa mapumziko wa Grand Bassam nchini Côte d'Ivoire, ambalo liliua watu 19 mwezi Machi 2016, wakiwemo raia wa Ulaya.

Washtakiwa wanne katika kesi ya shambulio la Grand-Bassam wamehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Washtakiwa wanne katika kesi ya shambulio la Grand-Bassam wamehukumiwa kifungo cha maisha jela. AFP - SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Mahakama imewakuta 'hatia' washtakiwa wanne waliokuwepo wakati kesi hiyo ikisikilizwa na 'kuwahukumu kifungo cha maisha', alitangaza hakimu Charles Bini.

Mahakama ilitekeleza ombi la mwendesha mashtaka wa umma Richard Adou, ambaye aliomba kifungo cha maisha wiki moja iliyopita.

Washtakiwa wanne waliokuwepo, Hantao Ag Mohamed Cissé, Sidi Mohamed Kounta, Mohamed Cissé na Hassan Barry, walishtakiwa kwa kuhusika katika shambulio hili kwa kuwasaidia wale wanaodhaniwa kuwa wahusika wakuu - ambao hawakuwepo wakati wa kesi,  mashataka ambayo wamekanusha.

Hati ya kimataifa ya kukamatwa imetolewa na mahakama dhidi ya Kounta Dallah, aliyewasilishwa kama mhusika mkuu wa operesheni ya shambulio hilo.

Mnamo Machi 13, 2016, washambuliaji watatu vijana walivamia ufuo wa Grand-Bassam, ambao ni maarufu sana kwa wageni, kisha wakavamia mikahawa kadhaa, wakiwafyatulia risasi wateja kabla ya kupigwa risasi na vikosi vya usalama.

Shambulio hili la wanajihadi ambalo lilidaiwa na tawi la Al-Qaeda katika Maghreb ya Kiislamu (Aqmi), ikiwa ni la kwanza kutokea nchini Côte d'Ivoire, liliua watu 19, wakiwemo Wafaransa wanne.

Raia tisa wa Côte d'Ivoire, raia mmoja Lebanon, Mjerumani mmoja, Mmasedonia mmoja, raia mmoja wa Mali, Mnigeria mmoja na mtu ambaye hakutambuliwa pia waliuawa katika shambulio hilo na watu 33 wa mataifa mbalimbali kujeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.