Pata taarifa kuu

MINUSMA: Côte d'Ivoire yatangaza kuondoa wanajeshi wake nchini Mali

Baada ya Ufaransa, Sweden na Uingereza, Côte d'Ivoire imetangaza kuondoa wanajeshi wake waliotumwa nchini Mali kama sehemu ya MINUSMA, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuleta utulivu nchini Mali. Jumla ya wanajeshi 900 kutoka Côte d'Ivoire wataondoka hatua kwa hatua nchini Mali ifikapo mwezi Agosti 2023.

Wanajeshi wa Côte d'Ivoire kutoka ujumbe wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, MINUSMA, wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 59 ya uhuru mjini Abidjan, Agosti 7, 2019.
Wanajeshi wa Côte d'Ivoire kutoka ujumbe wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, MINUSMA, wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 59 ya uhuru mjini Abidjan, Agosti 7, 2019. AFP - SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Côte d'Ivoire "inathibitisha kuwaondoa hatua kwa hatua wanajeshi na maafisa wa polisi waliotumwa katika kikosi cha MINUSMA", kulingana na barua iliyoandikwa na ujumbe wa kudumu wa Côte d'Ivoire kwa Umoja wa Mataifa na kutumwa kwa Jean-Pierre Lacroix, Naibu Katibu Mkuu wa Operesheni za Amani za Umoja wa Mataifa.

Wanajeshi wa mwisho wa Côte d'Ivoire wataondoka katika nchini Mali mnamo Agosti 2023.

Kujiondoa huku kunakuja wakati uhusiano wa kidiplomasia kati ya Mali na Côte d'Ivoire umezorota kwa kiasi kikubwa tangu kile kinachojulikana kama kesi ya "askari 49", askari waliokamatwa na kuwekwa chini ya kizuizi huko Bamako Julai 10.

Ikiwa watatu kati yao waliachiliwa, 46 bado wanazuiliwa nchini Mali, wakishutumiwa na mahakama za Mali kwa "jaribio la kuhatarisha usalama wa taifa". Serikali ya Mali pia inawashuku kuwa "mamluki" ambao dhamira yao ilikuwa kuyumbisha usalama wa nchi.

Kwa upande wake, Côte d'Ivoire imeendelea kukanusha shutuma hizi, na kuhakikisha kwamba askari hawa waliitwa katika shughuli za usaidizi wa vifaa kwa MINUSMA.

Togo imekuwa na nafasi ya mpatanishi kati ya Côte d'Ivoire na Mali tangu Julai 28, lakini mazungumzo bado hayajaza matunda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.