Pata taarifa kuu

Jaji wa Kiislamu aweka masharti ya kufungua tena shule Timbuktu

Jaji mashuhuri wa Kiislamu aliye karibu na kundi la al-Qaeda kaskazini mwa Mali ametoa masharti ya kufunguliwa tena kwa shule kwa kuwatenganisha wavulana na wasichana na kuwavika mavazi yanayolingana na Uislamu, kulingana na barua iliyothibitishwa Alhamisi na shirika la habari la AFP.

Katika moja ya mita ya Djingareyber, huko Timbuktu.
Katika moja ya mita ya Djingareyber, huko Timbuktu. © RFI/David Baché
Matangazo ya kibiashara

Katika barua hii iliyotumwa kwa gavana wa Timbuktu, cadi (jaji wa Kiislamu) pia anaomba "mamlaka za shule" kuanzisha visomo vya lugha ya Kiarabu na Quran shuleni.

Mfumo wa elimu wa Mali unashutumiwa vikali na makundi ya wanajihadi, katika maeneo makubwa ya vijijini ambako ushawishi wao ni mkubwa, kwa kutoheshimu sheria wanazozitetea, hasa kwa kutumia Kifaransa, kwa kutotenganisha wavulana na wasichana, kwa kuidhinisha nguo ambazo wanaziona kuwa ni kinyume na sheria zao. Jumla ya shule 1,766 zimefungwa nchini Mali, na kuathiri watoto nusu milioni, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ​​​​mwezi Oktoba.

Cadi huyo mashuhuri aliweka tarehe 26 Oktoba katika barua hii kwa gavana wa Timbuktu, mamlaka ya juu zaidi ya serikali katika eneo hilo, masharti haya matatu ya kufunguliwa tena kwa shule katika maeneo yaliyo chini ya ushawishi wa wanajihadi. Barua hiyo ilithibitishwa kwa shirika la habari la AFP na chanzo ndani ya jimbo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.