Pata taarifa kuu

Ivory Coast: Charles Blé Goudé kurejea nyumbani Novemba 26

Charles Blé Goudé, nguzo ya utawala wa rais wa zamani Laurent Gbagbo, aliliambia shirika la habari la AFP Jumatatu kwamba atarejea Côte d'Ivoire mnamo Novemba 26, baada ya kuachiliwa kwake mwaka jana na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) na kupata pasipoti mnamo mwezi Mei.

Charles Blé Goudé wakati ikitangazwa hukumu ya Kitengo cha Rufaa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Machi 31, 2021.
Charles Blé Goudé wakati ikitangazwa hukumu ya Kitengo cha Rufaa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Machi 31, 2021. © Capture d'écran ICC-CPI
Matangazo ya kibiashara

"Nitarejea nchini mwangu mnamo Novemba 26 na kushiriki katika mchakato wa maridhiano ambao ni muhimu kwa wananchi wenzangu," Charles Blé Goudé aliliambia shirika la habari la AFP.

Tarehe hii iliwekwa baada ya mkutano wa Jumatatu kati ya wajumbe kutoka chama cha Charles Blé Goudé na mkurugenzi katika ofisi ya  Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara.

"Imekubaliwa na mamlaka ya Côte d'Ivoire kwamba Charles Blé Goudé atarejea Côte d'Ivoire mnamo Novemba 26, 2022", inathibitisha taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa chama anachokiongoza, Pan-African Congress for Justice and Equality of Peoples ( Cojep ).

Charles Blé Goudé na Laurent Gbagbo waliachiliwa huru mwezi wa Machi 2021 na ICC huko Hague kwa madai ya uhalifu wakati wa mgogoro wa baada ya uchaguzi wa 2010-2011.

Wakati huo, ushindi wa urais wa Alassane Ouattara, uliopingwa na Laurent Gbagbo, ulisababisha mzozo wa baada ya uchaguzi ambao ulisababisha vifo vya watu 3,000 na kusababisha kukamatwa kwa Bw. Gbagbo mnamo Aprili 2011.

Charles Blé Goudé alikamatwa mwaka wa 2013 nchini Ghana, kisha kuhamishiwa Hague mwaka 2014 baada ya miezi kadhaa chini ya kizuizi cha nyumbani huko Abidjan.

Alipewa jina la utani la "mkuu wa barabara", kwa uwezo wake wa kuhamasisha umati wa watu na hasa vijana, kama kiongozi wa vuguvugu la kitaifa la wafuasi wa Gbagbo la Young Patriots.

Bw. Gbagbo aliweza kurejea Côte d'Ivoire mnamo Juni 2021, lakini Charles Blé Goudé alinyimwa pasipoti.

Alipata hati hiyo mwezi Mei lakini bado alikuwa akisubiri ruhsa kutoka kwa rais wa Côte d'Ivoire.

Laurent Gbagbo, alihukumiwa akiwa hayupo nchini Côte d'Ivoire kifungo cha miaka 20 jela kwa vitendo vinavyohusiana na mgogoro wa baada ya uchaguzi. Laurent Gbagbo alipata msamaha wa rais mwezi Agosti kuhusina na suala hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.