Pata taarifa kuu

Shirika lisilo la kiserikali la Uswisi la Geneva Call lapigwa marufuku nchini Mali

Shirika lisilo la kiserikali la Uswisi la Geneva Call limepigwa marufuku nchini Mali. Uamuzi uliochukuliwa na mamlaka ya mpito ya Mali Alhamisi, Desemba 15. Taarifa hii inatufikia hivi punde.

Marie Lequin, mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la ya Uswisii Geneva Call mnamo Juni 30, 2022 huko Kyiv.
Marie Lequin, mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la ya Uswisii Geneva Call mnamo Juni 30, 2022 huko Kyiv. © SERGEI SUPINSKY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Marufuku hii ya kufanya shughuli inakuja katika muktadha wa uimarishaji, unaofanywa na Bamako, wa udhibiti wa ufadhili na shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali, baada ya tangazo la kupiga marufuku, nchini Mali, kwa shughuli za ushirika zinazofadhiliwa au kuungwa mkono na Ufaransa. Hata hivyo, kupigwa marufuku kwa sirika lisilo la kierikali la Uswisi si jambo la msingi, linalohusishwa na hatua hii ya mshtuko iliyotangazwa karibu mwezi mmoja uliopita.

Agizo la kupiga marufuku shirka lisilo la kiserikali la Uswisi la Geneva Call limetiwa saini na Waziri wa Utawala wa Mali na msemaji wa serikali, Kanali Abdoulaye Maïga.

Hati hii, ya tarehe 15 Novemba, haitumii nakala yoyote rasmi kuhusu marufuku ya hivi karibuni ya mashirika yanayoungwa mkono na Ufaransa. Kwa upande wake, ni "shughuli zisizo halali", bila maelezo zaidi, ambayo inahalalisha rasmi marufuku hii ya kufanya shughuli nchini Mali.

Miongoni mwa hati zilizotajwa katika agizo hilo ni barua mbili za mwezi wa Oktoba: mazungumzo kati ya wizara ya Mali na shirika lisilo la kiserikali la Uswisi ambayo, kulingana na vyanzo vilivyohojiwa na RFI, yanahusu ziara ya ujumbe wa waasi wa zamani wa Azawad ( CMA) huko Geneva.

Ziara iliyofanyika miezi miwili na nusu iliyopita

Geneva Call ni shirika lililobobea katika kuheshimu ulinzi wa raia na makundi yenye silaha yasiyo ya serikali. Kwa hivyo, shirika hili liliwaalika wawakilishi wa CMA huko Geneva kwa ajili ya kutia saini, Septemba 30, "tendo la kujitolea" juu ya kuheshimu sheria za kibinadamu na hasa juu ya ulinzi wa wafanyakazi wa afya.

Waasi wa zamani wa kaskazini mwa Mali na mamlaka ya Bamako wamepatanishwa, kwenye karatasi tu, tangu kusainiwa kwa makubaliano ya amani ya 2015, lakini uhusiano wao - sio rahisi - umedorora sana tangu kuanza kwa utawala wa mpito nchini Mali, baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Agosti 2020. Leo, kutoaminiana kumeenea waziwazi.

Utawala wa mpito unaona kwamba kitendo cha shirika la Geneva Call cha kupatanisha pande hizo mbili ni kuingilia masuala ya ndani ya Mali na kuhatarisha usalama wa taifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.