Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Jeshi la Mali na wasaidizi wake kutoka Urusi wanyooshewa kidole kwa mauaji ya raia Kita

Nchini Mali, operesheni mpya ya jeshi la Mali na wasaidizi wake kutoka Urusi imegubikwa na shutuma za unyanyasaji. Operesheni hii Ilifanyika jana, Jumanne Desemba 6 asubuhi, huko Kita, kijiji cha wilaya ya Dioura, karibu na mpaka wa Mauritania. Ilikuwa siku ya soko. Vyanzo vya ndani vinathibitisha kuwa watu wawili hadi watano wameuawa na wengine kujeruhiwa. Kulingana na vyanzo hivi, waathiri wote ni raia wa kawaida.

Kulingana na vyanzo vilivyohojiwa na RFI, wanajeshi wa Mali na washirika wao kutoka Urusi walibaki Kita hadi alasiri, walifyatua risasi mara kadhaa kwenye umati wa watu, na kuua watu wanne au watano, kulingana na vyanzo hivyo.
Kulingana na vyanzo vilivyohojiwa na RFI, wanajeshi wa Mali na washirika wao kutoka Urusi walibaki Kita hadi alasiri, walifyatua risasi mara kadhaa kwenye umati wa watu, na kuua watu wanne au watano, kulingana na vyanzo hivyo. © Agnes COUDURIER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi wa Mali na washirika wao kutoka Urusi walifika asubuhi na mapema, mwanzoni mwa maonyesho ya kila wiki, wakiwa na helikopta kadhaa. Vikosi vya wanajeshi wa Mali (FAMA), kulingana na vyanzo kadhaa vya kuaminika vya ndani, viliambatana na wasaidizi wao kutoka Urusi, wakufunzi wa kawaida kulingana na serikali ya Bamako, mamluki wa kundi la Wagner kulingana na nchi nyingi za Magharibi na Afrika.

Wanajihadi kutoka Kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu (GSIM au Jnim kwa Kiarabu) wenye mafungamano na al-Qaeda wapo katika eneo hilo. Je, kwa kuingilia kati siku ya soko, jeshi la Mali - ambalo halikutaka kujibu maombi ya RFI - na wasaidizi wake wa Urusi walitaka kuchukua fursa ya kufanya mashambulizi? "Wangefanya vyema zaidi kuingilia kati pale ambapo wanajihadi walipo, badala ya kuja katikati ya soko," amelaumu mmoja wa viongozi wa kijiji cha Kita. Kwa sababu maonyesho ya kila wiki ya jiji hili, njia panda kati ya Mali na Mauritania, ni dhahiri hutembelewa na raia wengi.

Mkurugenzi wa kituo cha afya ajeruhiwa 

Kulingana na vyanzo vilivyohojiwa na RFI, wanajeshi wa Mali na washirika wao kutoka Urusi walibaki Kita hadi alasiri, walifyatua risasi mara kadhaa kwenye umati wa watu, na kuua watu wanne au watano, kulingana na vyanzo hivyo. Wanaume watatu walijeruhiwa, na kuhamishwa na wasafirishaji wa kiraia hadi Mauritania, na wengine wanane kukamatwa.

Pesa za maduka kadhaa pia zilichukuliwa na wanajeshi. Miongoni mwa waliofariki na kujeruhiwa ni wachuuzi wa mifugo na mkurugenzi wa kituo cha afya cha Kita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.