Pata taarifa kuu
AFRIKA YA MAGHARIBI- USALAMA

Mkutano wa 62 wa wakuu wa nchi za ECOWAS umeanza mjini Abuja Nigeria

Mkutano wa 62 wa wakuu wa nchi kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi, ECOWAS, wameanza kikao chao mjini Abuja Nigeria, huku masuala ya mapinduzi na vita dhidi ya makundi ya kijihadi, yakitawala ajenda za mkutano wa huu.

Bendera ya nchi za Jumuiya ya ECOWAS
Bendera ya nchi za Jumuiya ya ECOWAS © Wikicommons
Matangazo ya kibiashara

Katika kikao hiki, wakuu wan chi wamepokea ripoti ya tathmini iliyofanywa na jopo kazi maalum lililoundwa kushughulikia masuala ya Mali, Burkina Faso na Guinea, ambazo zilisimamishwa uanachama.

Awali ujumbe uliokuwa umetumwa katika mataifa hayo, ulisema uko tayari kushirikiana na kuzisaidia nchi hizo, lakini hawakubaliana na mapunduzi ya kijeshi yaliyofanyika.

Nchini Guinea, tayari serikali ya kipindi cha mpito cha miezi 24 imeunda lakini hatma yake haijulikani, huku nchini Burkina Faso, kiongozi mpya Ibrahim Traore akiwa hatabiriki.

Hali ya kisiasa nchini Mali, imesababisha mgogoro na mataifa jirani, huku vita dhidi ya makundi ya kijihadi, ikisuasua kutokana na uhaba wa fedha kusaidia vikosi vya G5 sahel, na kuingia kwa mamluki wa kigeni kwenye taifga hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.