Pata taarifa kuu

ECOWAS yaamua kuunda kikosi cha kikanda cha kupambana na wanajihad na mapinduzi

Maafisa wa kijeshi kutoka kanda hiyo watakutana mwezi Januari kujadili jinsi ya kuanzisha kikosi cha kikanda.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo, Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio, Mwenyekiti wa Tume ya ECOWAS Omar Alieu Touray, Waziri wa Jimbo Kuu la Shirikisho Mohammed Bello, wakati wa sherehe za uzinduzi wa sekretarieti mpya ya ECOWAS, huko Abuja, Nigeria Desemba 4, 2022.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo, Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio, Mwenyekiti wa Tume ya ECOWAS Omar Alieu Touray, Waziri wa Jimbo Kuu la Shirikisho Mohammed Bello, wakati wa sherehe za uzinduzi wa sekretarieti mpya ya ECOWAS, huko Abuja, Nigeria Desemba 4, 2022. REUTERS - AFOLABI SOTUNDE
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Afrika Magharibi waliamua siku ya Jumapili mjini Abuja, Nigeria, kuunda kikosi cha kikanda kitakachojitolea kuingilia kati sio tu dhidi ya wanajihadi lakini pia katika tukio la mapinduzi, wakati kanda hiyoinashuhudia matukio kadhaa ya mapinduzi kwa miaka miwili, alisema afisa mmoja mwandamizi.

Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) au wawakilishi wao waliokutana katika mkutano huo pia walitaka utawala wa kijeshi nchini Mali kuwaachilia huru kabla ya Januari 1, wanajeshi 46 wa Côte d'Ivoire wanaozuiliwa tangu mwezi Julai, Omar Touray, Mwenyekiti wa tume ya ECOWAS, aliwaambia waandishi wa habari.

Vinginevyo, ECOWAS itachukua vikwazo, mwanadiplomasia wa Afrika Magharibi alimwambia mwandishi wa shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina, wakati kesi hii ni chanzo cha mvutano mkubwa kati ya Mali na Côte d'Ivoire.

Rais wa Togo Faure Gnassingbé, ambaye ana majukumu makubwa katika mzozo huu, atasafiri kwenda Mali "kudai" kuachiliwa kwa wanajeshi hao, aliongeza mwanadiplomasia huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.