Pata taarifa kuu

Rais wa ECOWAS Umaro Sissoco Embalo azuru Moscow kisha Kyiv

Rais wa sasa wa ECOWAS Umaro Sissoco Embalo anaanza ziara rasmi huko Moscow Jumatatu, Oktoba 24. Pia rais wa Guinea-Bissau, ndiye rais wa pili kutoka Afrika kupokelewa na Vladimir Putin, baada ya rais wa Umoja wa Afrika na pia rais wa Senegal Macky Sall, ambaye alikwenda Sochi kuomba kusitishwa kwa vikwazo vya bandari za Ukraine chanzo cha kupanda kwa bei ya vyakula. Umaro Sissoco Embalo kisha atasafiri kwenda Kyiv, nchini Ukraine.

Rais wa Guinea-Bissau na Rais wa sasa wa ECOWAS Umaro Sissoco Embalo, hapa ni wakati alipozuru Paris mnamo Oktoba 3, 2022.
Rais wa Guinea-Bissau na Rais wa sasa wa ECOWAS Umaro Sissoco Embalo, hapa ni wakati alipozuru Paris mnamo Oktoba 3, 2022. © Ludovic Marin / AFP
Matangazo ya kibiashara

Je, Urusi inataka kuvutia ECOWAS kwa upande wake baada ya ziara ya mapema mwezi Oktoba ya mkuu wa diplomasia ya Ukraine Dmytro Kuleba kwenda Dakar na Abidjan? Uhusiano kati ya Urusi na baadhi ya nchi za Kiafrika zenye urafiki wa jadi una historia ndefu. Nchi nyingi za Kiafrika, hasa zilizokuwa makoloni ya Ureno, zimejenga uhusiano wa karibu na Umoja wa Kisovieti. Na Moscow leo inanufaika leo na enzi hizo zilizopita.

Wakati Urusi ilipoivamia Ukraine mwezi Februari, karibu nusu ya nchi za Afrika zilijizuia kusema hohote, tofauti na jumuiya nyingi za kimataifa. Je, rais wa  Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo angetaka kurekebisha hali hii, akiwa amebeba katika sanduku lake ujumbe wa amani kwa niaba ya jumuiya nzima ya Afrika Magharibi:

Ninaenda Urusi Jumatatu hii, nitakuwa na Rais Vladimir Putin. Ninamfikishia ujumbe wa amani. Nitamwambia kwamba ni muhimu kuzungumza na kaka yake [Volodymyr] Zelensky. Mara nyingi mimi huzungumza na Zelensky, kama Emmanuel Macron kuhusiana na suala hili. Mimi ni rais wa pili wa Afrika baada ya Rais Macky Sall, mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika, kwenda Urusi. Siendi kama rais wa Guinea-Bissau, lakini kama rais wa sasa wa ECOWAS, kumweleza Putin kwamba ni muhimu kuzungumzia amani kwa sababu dunia ina matatizo mengi.

Baada ya Moscow, Umaro Sissoco Embalo pia atazuru Kyiv kama sehemu ya misheni hii ya amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.