Pata taarifa kuu

Emmanuel Macron adai amani nchini Ukraine 'inawezekana' wakati Waukraine 'wataamua'

Rais wa Ufaransa alizungumza Jumapili hii, Oktoba 23 katika ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa amani ulioandaliwa mjini Roma na jumuiya ya Kikatoliki ya Sant'Egidio.

Huko Roma, Emmanuel Macron ametangaza kwamba ilikuwa muhimu kuwa na "ujasiri" wa "kutaka amani".
Huko Roma, Emmanuel Macron ametangaza kwamba ilikuwa muhimu kuwa na "ujasiri" wa "kutaka amani". AP - Alessandra Tarantino
Matangazo ya kibiashara

"Wakati fulani, kulingana na jinsi mambo yanavyoendelea na wakati raia wa Ukraine na viongozi wao wameamua, kwa masharti waliyoamua, amani itajengwa na mwingine, ambaye ni adui wa 'leo, kwenye meza ya mazungumzo," amesema Emmanuel Macron wakati wa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa amani ulioandaliwa na jumuiya ya Kikatoliki ,nchini Italia ya Sant'Egidio.

"Amani haiwezi kuwa sheria ya wenye nguvu zaidi", amesisitiza rais wa Ufaransa. "Wakraine wanapigania kuokoa uhuru wao," amekumbusha. "Amani inawezekana, lakini wakati Waukraine wataamua na wakati wataheshimu utu huu na uhuru huu".

Huku akiiunga mkono Ukraine kidiplomasia na kijeshi, mkuu wa nchi wa Ufaransa ameendelea tangu kuanza kwa mzozo wa Ukraine mwezi Februari kumsihi raisa wa Ukraine kuzungumza na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, tofauti na viongozi wengine wa nchi za Magharibi na hasa rais wa Marekani Joe Biden. Aliomba tena, siku ya Ijumaa huko Brussels, Kyiv na Moscow kurudi "kwenye meza ya mazungumzo" wakati "itakubalika" kwa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky - lakini pia "haraka iwezekanavyo".

Msimamo huu wakati mwingine umekosolewa na Emmanuel Macron amechukua fursa ya hotuba yake ya Jumapili kuhalalisha mbele ya mamia ya viongozi wa kisiasa na kidini kutoka kote ulimwenguni waliokusanyika kwa kongamano hili la siku tatu. "Kuzungumza juu ya amani na wito wa amani leo kunaweza kuwa na kitu kisichoweza kuvumiliwa kwa wale wanaopigania uhuru wao, na kuwapa (wao) hisia ya kusalitiwa kwa namna fulani", hivyo kutambuliwa rais wa Ufaransa. Lakini alisisitiza haja ya kuwa na "ujasiri" wa "kutaka amani", hata kama "kuwaza amani wakati wa vita" ni "kubwa zaidi ya isiyofikirika".

Rais wa Ufaransa amewasili Roma Jumapili alasiri, ambapo atapokelewa Jumatatu hii asubuhi na Papa Francis kwa hadhira ya faragha huko Vatican, wa tatu kati ya watu hao wawili tangu kuchaguliwa kwa Emmanuel Macron mnamo 2017 Mwishoni mwa mkutano wake wa faragha, hotuba yake, alifichua kwamba atamkabidhi papa toleo la Mradi wa Amani ya Milele wa Immanuel Kant.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.