Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Nigeria: 'Mke wa Rais afuta malalamiko yake' mahakamani dhidi ya mwanafunzi

Chama cha kitaifa cha wanafunzi wa Nigeria kilikuwa kimeitisha maandamano ya kitaifa kuanzia tarehe 5 Desemba 2022.

Siku ya Alhamisi, wakili Agu alibaini kwamba kijana huyo alifikishwa siku mbili mapema mbele ya mahakama ya jinai huko Abuja kwa "kuchafua jina" (shitaka linaloadhibiwa miaka miwili jela kwa mujibu wa kanuni ya adhabu ya Nigeria) kufuatia malalamiko ya mke wa Rais Muhammadu Buhari.
Siku ya Alhamisi, wakili Agu alibaini kwamba kijana huyo alifikishwa siku mbili mapema mbele ya mahakama ya jinai huko Abuja kwa "kuchafua jina" (shitaka linaloadhibiwa miaka miwili jela kwa mujibu wa kanuni ya adhabu ya Nigeria) kufuatia malalamiko ya mke wa Rais Muhammadu Buhari. © daily Trust
Matangazo ya kibiashara

Mke wa rais wa Nigeria ameondoa malalamiko yake ya kashfa iliyomfanya mwanafunzi mmoja kufikishwa mahakamani hivi majuzi kufuatia ujumbe wa Twitter ambao aliuona kuwa wa kuudhi, upande wa utetezi wa kijana huyo ulibaini siku ya Ijumaa.

"Mke wa Rais ameondoa malalamiko yake," Chiejoke Agu, wakili wa Aminu Adamu, mwanafunzi ambaye kukamatwa kwake Novemba 18 kwa sababu ya ujumbe kwenye Twitter ulioonekana kumtusi Bi Aisha Buhari, na hivyo kitendo hiki cha kukamatwa kililaaniwa na kutajwa kwa  "kinyume cha sheria" na shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International.

Kulingana na chanzo cha mahakama, "mshtakiwa ataachiliwa kwa dakika yoyote. Hati za kuachiliwa kwake zinashughulikiwa".

Mwanafunzi katika chuo kikuu kaskazini mwa Nigeria, Bw. Adamu, aliyezaliwa mwaka wa 1998, alikamatwa miezi mitano baada ya kutuma ujumbe kwenye Twitter ambapo alitoa maoni yake kuhusu sura ya Aisha Buhari, mke wa rais Muhammadu Buhari'.

Siku ya Alhamisi, wakili Agu alibaini kwamba kijana huyo alifikishwa siku mbili mapema mbele ya mahakama ya jinai huko Abuja kwa "kuchafua jina" (shitaka linaloadhibiwa miaka miwili jela kwa mujibu wa kanuni ya adhabu ya Nigeria) kufuatia malalamiko ya mke wa Rais Muhammadu Buhari.

Chama cha Kitaifa cha Wanafunzi wa Nigeria (NANS) kilikuwa kimeitisha maandamano kote nchini kuanzia tarehe 5 Desemba "hadi (kuachiliwa) bila masharti" kwa Bw. Adamu.

Kiongozi wa chama hiki, Felix Atah, alikaribisha siku ya Ijumaa tangazo kwamba malalamiko ya Bi Buhari yaliondolewa, kwa wakati ufaao, alisema, kwa mwanafunzi huyo kufanya "mitihani yake ya mwisho inayoanza Jumatatu".

Shirika la Amnesty International, ambalo lilidai kuachiliwa "haraka" kwa Bwana Adamu, liliandika Jumapili kwamba mwanafunzi huyo "amepigwa, kuteswa na aina nyingine za unyanyasaji", kulingana na taarifa kutoka kwa familia yake na marafiki. .

Katika miaka ya hivi karibuni, ukosoaji kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu umeongezeka dhidi ya mamlaka ya Nigeria, ikishutumiwa hasa kwa mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya uhuru wa kujieleza na kutoa maoni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.