Pata taarifa kuu

Mwanafunzi afikishwa mahakamani kwa kumtusi mke wa rais wa Nigeria

Mwanafunzi mmoja nchini Nigeria amefikishwa mbele ya mahakama ya jinai mjini Abuja kwa kumkashifu mke wa rais wa nchi hiyo Aisa Buhari, kwa sababu ya ujumbe wa Twitter unaoonekana kumkera, wakili wake ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Alhamisi.

Mke wa rais wa Nigeria, Aisha Buhari.
Mke wa rais wa Nigeria, Aisha Buhari. TWITTER/AISHA M. BUHARI
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama amzo shirika la habari la AFP limepata kopi, Aminu Adamu, aliyezaliwa mwaka 1998 na mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Shirikisho cha Dutse, kaskazini mwa Nigeria, alikamatwa Novemba 18 na kuhamishiwa Abuja, miezi mitano baada ya kutuma ujumbe huu akitoa maoni yake kuhusu sura ya mke wa rais, Aisha Buhari, na kumlaumu kwa "kula pesa za maskini".

Kukamatwa kwake, kuliolaaniwa vikali na shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International, kulifuatia uchunguzi wa awali uliofanywa na polisi baada ya kuwasilisha malalamiko ya mke wa Rais Muhammadu Buhari, kulingana na hati hizi na chanzo cha mahakama.

Kijana huyo "alifikishwa Jumanne" mbele ya mahakama ya jinai ya mwanzo katika eneo la Federal Capital Territory (FCT), wakili wake Chijioke Agu ameliambia shirika la habari la AFP kwa simu. "Anakabiliwa na mashitaka ya kukashifu," amesema. Kulingana na kanuni ya adhabu ya Nigeria, Bw. Adamu anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka miwili jela.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Januari 30, 2à23 amesema Bw. Agu, na kuongeza kuwa amewasilisha ombi la dhamana kwa mteja wake, ambaye anazuiliwa katika gereza la Suleja, kaskazini magharibi mwa Abuja.

Kulingana na stakabadhi za mahakama zilizoonwa na shirika la habari la AFP, mwanafunzi huyo alikiri kutuma ujumbe huo wa kukera kwenye ukurasa wake wa Twitter, ambao ulijumuisha picha ya Bi Buhari na maoni yake katika lugha ya Kihausa, lugha inayozungumzwa zaidi kaskazini mwa Nigeria.

Katika taarifa iliyotolewa Jumapili, Amnesty International iliandika kwamba familia na jamaa wa Bw. Adamu wanadai kwamba "alipigwa, kuteswa na aina nyingine za unyanyasaji". Amnesty pia imeshutumu "kukamatwa kwa kijana huyo kinyume cha sheria", na kutaka kuachiliwa kwake "mara moja" na "bila masharti".

Chini ya masharti ya Katiba, Bw. Buhari ataondoka madarakani mwaka wa 2023 baada ya kuhudumu kwa mihula miwili kama rais wa Nigeria. Katika miaka ya hivi karibuni, mashirika ya kutetea haki za binadamu yamezidisha ukosoaji dhidi ya serikali, ambayo wanaishutumu hasa kwa mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya uhuru wa kujieleza na maoni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.