Pata taarifa kuu

Somalia: Mamlaka yachukua tena udhibiti wa hoteli iliyoshambuliwa na Al Shabab mjini Mogadishu

Nchini Somalia, hoteli iliyo katikati mwa Mogadishu, ambako watu wa ngazi za juu wanaishi, ililengwa tangu Jumapili jioni na Al Shabab. Msemaji wa polisi ametangaza, mchana wa Jumatatu, Novemba 28, kumalizika kwa operesheni operesheni ya polisi ambayo ilikuwa imezingira hoteli hiyo. Idadi ya vifo ni angalau raia wanane, kulingana na polisi.

Gari ya wagonjwa mahututi iliyokuwa imebeba mtu aliyejeruhiwa katika hospitali ya Kalkaal kufuatia shambulio la Al habab dhidi ya hoteli Villa Rose huko Mogadishu, Somalia, Novemba 28, 2022.
Gari ya wagonjwa mahututi iliyokuwa imebeba mtu aliyejeruhiwa katika hospitali ya Kalkaal kufuatia shambulio la Al habab dhidi ya hoteli Villa Rose huko Mogadishu, Somalia, Novemba 28, 2022. REUTERS - FEISAL OMAR
Matangazo ya kibiashara

Operesheni ya polisi ya kuzingirwa hoteli hiyo imalizika katikati ya alasiri, ametangaza msemaji wa polisi, akinukuliwa na shirika la habari la AFP. Operesheni hiyo itakuwa imechukua karibu saa 20.

"Operesheni ya polisi katika hoteli ya Villa Rose imemalizika," msemaji wa polisi Sadik Dudishe amewaambia waandishi wa habari. Al Shabab "waliua raia 8 waliokuwa katika hoteli hiyo na vikosi vya usalama vimefanikiwa kuwaokoa takriban 60 kati yao, na hakuna hata mmoja aliyejeruhiwa", amesema Bw. Dudishe na kuongeza kuwa askari mmoja wa vikosi vya usalama pia ameuawa.

Msemaji wa polisi ya Somalia amesema shambulio hilo lilitekelezwa kwa karibu saa 21 na watu sita na "watano walipigwa risasi na mmoja akajilipua". Shambulio hilo lilianza Jumapili jioni kwa njia ya kawaida kabisa. Bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari lililipuka kwenye lango la hoteli hiyo kabla ya mmoja kati ya washambuliaji mmoja kupenya na kufanikiwa kuingia ndani ya hoteli ambayo kawaida kuwa huwa chini ya ulinzi mkali.

Baada ya hoteli Hayat msimu huu wa joto, ilikuwa zamu ya hoteli Villa Rose, hoteli maarufu sana kwa maafisa wakuu na wabunge, iliyoko karibu na ikulu ya rais ya Villa Somalia, ambayo ililengwa.

Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, angalau waziri mmoja alijeruhiwa. Adam Haw Hirsi, Waziri wa Mazingira, ametangaza kwenye ukurasa wake wa Twitter, Jumapili jioni, kuwa salama salimini. Maafisa wa serikali walifanikiwa kutoroka kupitia madirisha ya hoteli hiyo.

Mtaa huo ulikuwa umezingirwa na vikosi vya usalama. Milio ya risasi na milipuko ilisikika Jumatatu asubuhi. Kulingana na afisa wa idara ya usalama ya Somalia, aliyehojiwaa na shirika la habari la AFP, washambuliaji "walikwama kwenye chumba cha jengo" ambapo vikosi vya usalama vilifanikiwa kuwatimua mchana.

Idadi ya hivi punde inaripoti kuwa takriban raia wanane waliuawa. Polisi pia imeongeza kuwa shambulio hilo lilitekelezwa na watu sita, "watano kati yao walipigwa risasi na mmoja alijilipua".

Shambulio hili jipya linakuja wakati Rais Hassan Cheikh Mohamoud aliamua msimu uliopita wa kiangazi kushiriki katika "vita kamili" dhidi ya Al Shabab.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.