Pata taarifa kuu

Washington yatoa dola milioni 10 kwa taarifa kuhusu Al Shabab

Marekani imetangaza Jumatatu kuongeza hadi dola milioni 10 kama zawadi itayowezesha kuwapata viongozi watatu wa Al Shaba nchini Somalia, nchi iliyokabiliwa na mashambulizi ya umwagaji damu ya kundi la Kiislamu lenye itikadi kali katika wiki za hivi karibuni.

Al Shabab walifukuzwa kutoka katika miji mikuu ikiwa ni pamoja na Mogadishu mwaka 2011 lakini wamebaki imara katika maeneo makubwa ya vijijini ambako wanafanya mashambulizi hasa dhidi ya vikosi vya usalama na ulinzi pamona na  maafisa wa serikali.
Al Shabab walifukuzwa kutoka katika miji mikuu ikiwa ni pamoja na Mogadishu mwaka 2011 lakini wamebaki imara katika maeneo makubwa ya vijijini ambako wanafanya mashambulizi hasa dhidi ya vikosi vya usalama na ulinzi pamona na maafisa wa serikali. REUTERS / Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

"Programu ya Tuzo ya Wizara ya Sheria ya Marekani inaongeza kitita chake cha zawadi hadi Milioni 10 kwa kila moja ya habari zitakayosaidia kutambuliwa au mahali pa waliopo viongozi wakuu wa Al-Shabab Ahmed Diriye, Mahad Karate na Jehad Mostafa," imebaini taarifa kutoka kwa Ubalozi wa Marekani nchini Kenya.

Zawadi hii pia inatumika kwa taarifa yoyote "itayosababisha kutatizika kwa mifumo ya kifedha ya Al Shabab", umeongeza ubalozi wa Marekani. Hii ni "mara ya kwanza kwa wizara ya sheria ya Marekani kutoa zawadi kwa taarifa kuhusu mitandao ya kifedha ya Al-Shabab," aliongeza.

Ahmed Diriye ni kiongozi wa Al Shabab, kundi la Kiislamu linalohusishwa na Al Qaeda tangu 2014, ambalo limekuwa likiongoza uasi dhidi ya serikali ya shirikisho kwa miaka 15 ili kuanzisha sheria za Kiislamu nchini Somalia. Alilengwa hadi sasa na zawadi ya dola milioni sita. Mahad Karate anachukuliwa kuwa nambari 2 yakundi hili.

Jehad Mostafa, raia wa Marekani aliyeishi California, anachukuliwa kuwa mmoja wa wakufunzi wakuu wa kijeshi na "kiongozi wa matumizi ya vilipuzi" kwa mashambulizi. "FBI inaamini kwamba Mostafa ndiye gaidi wa cheo cha juu zaidi wa utaifa wa Marekani anayepigana nje ya nchi," ubalozi umesema.

Tangazo hili linakuja wakati Somalia inakabiliwa na umwagaji damu tena wa mashambulizi ya Al Shaba, ambao wameapa kuifuta serikali ya shirikisho inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.

Shambulizi la hivi punde, la mabomu mawili lililotegwa kwenye magari katika mji mkuu wa Mogadishu mnamo Oktoba 30, lilisababisha vifo vya watu 121 na 333 kujeruhiwa kulingana na Umoja wa Mataifa ukitoa takwimu rasmi za Somalia siku ya Jumatatu, shambulio baya zaidi kuwahi kutokea nchini humo tangu mwaka 2017.

Siku ya Jumatatu, Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk, amesema zaidi ya raia 600 wameuawa mwaka huu katika mashambulizi ya kundi hilo katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika iliyo katika hali tete. Hii ndiyo idadi ya juu zaidi tangu mwaka 2017 na ongezeko la zaidi ya 30% ikilinganishwa na mwaka 2021.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamoud alikuwa ameahidi "vita vya hali ya juu" katikati ya mwezi wa Agosti kuwaangamiza Al Shabab na kuwataka wakazi "kujiepusha" na maeneo yanayodhibitiwa na Waislam ambao walikuwa wakilengwa na mashambulizi ya siku zijazo, baada ya shambulio la umwagaji damu lililodumu kwa zaidi ya saa thelathini dhidi ya hoteli moja mjini Mogadishu, shambulio ambalo lilisababisha vifo vya takriban watu 21 na 117 kujeruhiwa.

Al Shabab walifukuzwa kutoka katika miji mikuu ikiwa ni pamoja na Mogadishu mwaka 2011 lakini wamebaki imara katika maeneo makubwa ya vijijini ambako wanafanya mashambulizi hasa dhidi ya vikosi vya usalama na ulinzi pamona na Β maafisa wa serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.