Pata taarifa kuu

Somalia: Wanne wafariki baada ya Hoteli moja iliyoshambuliwa na Al Shabab kuzingirwa Mogadishu

Raia wengi na wanasiasa wameokolewa na kuhamishwa kutoka hoteli Villa Rose mjini Mogadishu. Takriban watu wanne wameuawa baada ya Hoteli Villa Rose iliyoshambuliwa na Al Shabab kuzingirwa huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, Hoteli ambayo inakaliwa kwa mabavu tangu Jumapili jioni na wapiganaji wa kijihadi wa Al Shabab, kulingana na afisa wa huduma za usalama za Somalia.

Vikosi vya usalama karibu na hoteli Hayat huko Mogadishu, katika mji mkuu wa Somalia, tarehe 21 Agosti 2022. Hoteli hiyo ilishambuliwa na Al Shabab.
Vikosi vya usalama karibu na hoteli Hayat huko Mogadishu, katika mji mkuu wa Somalia, tarehe 21 Agosti 2022. Hoteli hiyo ilishambuliwa na Al Shabab. © Farah Abdi Warsameh/AP
Matangazo ya kibiashara

"Magaidi wamekwama katika chumba cha jengo na vikosi vya usalama vinakaribia kukomesha operesheni hiyo haraka sana," ameongeza Mohamed Dahir, bila kutoa utambulisho wa wahanga hao waliouawa.

Hoteli Villa Rose, inatumiwa na maafisa wa serikali katikati mwa mji wa  Mogadishu.

Milio ya risasi na milipuko ya hapa na pale ilikuwa bado ikisikika wakati wa jua lilipokuwa likichomoza karibu na hoteli hii, maarufu kwa wabunge na maafisa wakuu, na iliyoko mita chache chache kutoka ofisi ya Rais Hassan Cheikh Mohamoud.

"Kundi la wapiganaji wa Al-Shabab walishambulia hoteli katika wilaya ya Bondhere usiku wa leo (na) vikosi vya usalama vinashiriki kuwaondoa," msemaji wa polisi wa kitaifa Sadik Dudishe alisema katika taarifa siku ya Jumapili.

Raia wengi na wanasiasa waliokolewa na kuhamishwa Jumapili jioni.

"Nilikuwa karibu na Hoteli Villa Rose wakati milipuko miwili mikali ilipotikisa hoteli. Kulikuwa na ufyatuaji risasi mkubwa. Eneo lilikuwa limezingirwa na nikaona watu wakikimbia," amesema shahidi Aadan Hussein kutoka Mogadishu.

Al Shabab, kundi lenye mafungamano na al-Qaeda ambalo limekuwa likijaribu kupindua serikali kuu ya Somalia kwa miaka 15, lilidai kuhusika na shambulio hilo.

Jeshi la Umoja wa Afrika nchini Somalia (Atmis) limelaani shambulio hilo na "kupongeza" kwenye Twitter "vikosi vya usalama vya Somalia kwa hatua yao ya haraka ya kuzuia majeruhi zaidi na uharibifu wa mali".

Mashambulio ya kulipiza kisasi

Shambulio hili jipya linakuja wakati rais wa Somalia, aliyechaguliwa mwezi Mei, ameamua kushiriki kwa miezi mitatu katika "vita kamili" dhidi ya Al Shabab.

Jeshi la Somalia, likisaidiwa na kabila mbalimali nchini humo, na Atmis, na kwa msaada wa mashambulizi ya anga ya Marekani, wameweza kudhibiti tena jimbo la Hiran na maeneo makubwa ya Shabelle ya Kati, katikati mwa nchi.

Lakini waasi hao walilipiza kisasi kwa mfululizo wa mashambulizi ya umwagaji damu, wakisisitiza uwezo wao wa kushambulia katikati ya miji ya Somalia na mitambo ya kijeshi.

Mnamo Oktoba 29, magari mawili yaliyokuwa na vilipuzi yalilipuka kwa dakika chache mjini Mogadishu, na kuua watu 121 na wengine 333 kujeruhiwa. Shambulio baya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka mitano katika nchi hii iliyoko katika Pembe ya Afrika.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, takriban raia 613 tayari wameuawa na 948 kujeruhiwa katika ghasia za mwaka huu nchini Somalia, hasa zilizosababishwa na vilipuzi (IEDs) vinavyohusishwa na Al-Shabab. Idadi kubwa zaidi tangu 2017, na zaidi ya 30% kutoka 2021.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.